Waziri wa Vijana ashiriki katika maadhimisho ya mfuko wa "Tahya Masr" kwa usajili rekodi mpya ya Guinness


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishiriki kwenye maadhimisho ya mfuko wa "Tahya Masr" kwa kusajili rekodi mpya katika Elezo la Guinness, huko ngome ya Salah El-Din Al-Ayoubi, chini ya wiki moja baada ya kusajili rekodi mbili katika Elezo hilo,ili uwe wenye  mataji matatu ya ulimwengu baada ya uandaaji wake msafara mkubwa zaidi wa misaada ya kibinadamu ulimwenguni.


Wakati wa maadhimisho hayo, Waziri wa Michezo na mawaziri walioshiriki walishuhudia filamu ya maandishi kuhusu jaribio la mfuko wa "Tahya Masr" kwenye kusajili rekodi kwenye Elezo la Guinness la kimataifa, pamoja na sehemu ya muziki ya kikundi cha Opera.


Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Mohammed Amin Nasr, mshauri wa Rais wa Masuala ya Kifedha na Mweka Hazina wa mfuko wa "Tahya Masr", mawaziri wa vijana na michezo, utalii, mambo ya kale, mipango na maendeleo ya uchumi, mshikamano wa jamii, vyombo vya habari, ushirikiano wa kimataifa, viwanda na Biashara, Afya na Elimu, pamoja na idadi kubwa ya mawaziri na magavana wa zamani, mwakilishi wa kikanda wa Guinness World Records na mabalozi kadhaa wa nchi za nje.


Wakati wa sherehe hiyo, Ashraf Sobhy alisisitiza madai yake juu ya uwezo wa nchi ya Misri kwenye kuonekana katika vikao vya kimataifa katika nyanja tofauti, hapo awali Waziri alipokuwa ameshuhudia mafanikio ya Misri ya mafanikio mapya katika Elezo la Guinness kwa kuruka juu kabisa kutoka kwa maji kwenye mwogeleaji  Mmisri Omar Sayed Shaaban, mchezaji wa timu ya kitaifa ya kuogelea na mapenzi.


Mfuko wa "Tahya Masr" ilizindua kauli mbiu yake mpya" Tunashirikiana kwa ajili ya ubinadamu" kuhamasisha vyama vya kazi za jamii ulimwenguni kote kufikia idadi ya rekodi katika kazi ya hisani na mshikamano kuhudumia ubinadamu.


Sherehe hiyo, Ngome ya Salah El-Din Al-Ayoubi na Borg khalifa huko Emirate ya Dubai zitawashwa kwa jina la kauli mbiu mpya kwa kushirikiana na wizara ya utalii na mambo ya kale.


Ikumbukwe kuwa mfuko wa "Tahya Masr" ulisajili rekodi mbili katika Guinness World Records, baada ya kufanikiwa uaandaji msafara mkubwa zaidi unaotoa katoni za chakula ulimwenguni na idadi mpya ndio lori kubwa zaidi la misaada ya kibinadamu duniani.

Comments