Mawaziri wa vijana na mshikamano washuhudia sherehe ya " ndoto yako yatekelezwa " kwa walemavu

Dokta Ashrf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo , Dokta Neveen El-qubak, Waziri wa mshikamano wa kijamii, siku ya Jumamosi, walishuhudia  sherehe ya " ndoto yako yatekelezwa " iliyofanywa na mpango wa " Alaam Muwazi" kwenye kitivo cha elimu chuo kikuu cha Ain Shams kwa maadhimisho ya siku ya ulimwengu kwa watu walemavu, na hivyo katika mfumo wa kutilia mkazo mifano inayon'gaa ya watu walemavu na kusisitizia umuhimu wa jukumu lao katika jamii .


sherehe ilijumuisha Tangazo la kuzindua tamthilia ya kidrama na kijamii inayoangazia  watu wenye uwezo maalum "ulemavu " ina jina la " kesi 404 " . vilevile ,  kuzindua vipindi viwili vya Vyombo vya habari ili kugusa changamoto na matatizo yote yanayokumba  walemavu na kuonesha njia ya kuwaunganisha na ufanisi wao katika jamii , mpango wa " Alaam Muwazi " unakumbatia kazi za kisanaa na vyombo vya habari, kwa ajili ya kuhakikisha fursa nzuri kwa nyota na mabingwa walemavu katika nyanja ya kisanaa na vyombo vya habari.


Katika kauli yake, Waziri wa vijana na michezo alielezea furaha yake kushiriki katika sherehe ya "ndoto yako yatekelezwa " na ambayo anwani yake inaashiria kutekeleza matumaini na matakwa ya wana wa Misri wa watu walemavu katika nyanja mbalimbali kwa kushirikiana na juhudi za taasisi na mamlaka zote zinazohusika , katika upande wa utiliaji mkazo wa Mheshimiwa :- Rais Abd El-Fatah El-Sisi Rais wa Jamhuri kwa kuunga mkono na kutunza kundi hilo na kutosheleza mahitaji na matakwa yao  pamoja na kuwajihusisha  katika miradi na shughuli mbalimbali.


Sobhy aliongeza akisema kwamba Wizara ya vijana na michezo inachukua jukumu pekee kwa watu walemavu kutokana na imani kwa uwezo wao wa kukabiliana  na lolote na kufikia kwao mafanikio katika nyanja mbalimbali , na  Wizara inaongeza programu na shughuli zinazohusiana nao katika maeneo ya vijana na michezo  yanayoenezwa kwenye mikoa ya Jamhuri , na kufanya kazi ya kuwajihusisha katika shughuli zinazofanywa mnamo mwaka mzima , akisifu kupambanua vipaji vya pekee vya wenye uwezo maalum Ema katika uwanja wa kisanaa au michezo au vyombo vya habari au nyinginezo.


 Waziri huyo alielekeza Shukrani na uthamini kwa wanaohusika  wa mpango " Alaam Muwazi"  kulingana na mihangaiko ya kutunza watu walemavu kuangazia vipaji vyao na kugusa mambo yote yanayowahusika   na hivyo kwa kuambatana na taasisi tofauti zinazohusika.


Comments