Misri yashiriki katika duru ya mazoezi ya kwanza kwa wachezaji mabingwa wa olimpiki ya ulemavu

Katika kipindi cha siku mbili , jukwaa la mtandao linazinduliwa kwa kutumia mbinu wa Zoom,  duru  ya  mazoezi ya kikanda ya kwanza kwa wachezaji mabingwa wawe kama wawakilishi wa Afya ya olimpiki maalum na hiyo kwa ushirikiano wa Misri na nchi za kiarabu 11 nazo ni Jordani , Syria , UAE , Morocco , Tunisia ,   Algeria , Mauritania , kuwait , Oman , Baharini  na Lebanon . 


Idadi ya washiriki katika duru ile inafikia wachezaji mabingwa 69 walio wawakilishi wa Afya pamoja na wenzao ( wachezaji mabingwa 49  - wafuatiliaji 20 ) , na kama inavyosemekana na " Nibeal Fatuni" ambaye ni mkurugenzi wa mipango kwenye uongozi wa kikanda kuwa duru hiyo inakuja  miongoni mwa mpango wa shughuli za mwaka ulioandikishwa na Mhandisi " Ayman Abdelwahab"  Mkuu wa kikanda  na japo Janga la Corona ila  shughuli haisitishwi mitandaoni  na hiyo ni duru ya kwanza katika uwanja huo.


Lela El-shnawy, Mkurugenzi wa mifumo ya kiafya  alisema kuwa  programu ya mchezaji bingwa ambaye ni mwakilishi wa Afya huyo ni mchezaji katika olimpiki maalum hufundishwa ili awe  mwakilishi wa Afya na ukuzaji wa misuli na mfano bora wa wachezaji  katika jamii  yake ya ndani . Na  kwamba masuala  yatakayoguswa  yanajumuisha :- uzima wa misuli , maelezo juu ya Janga la Corona , lishe na Chakula cha kiafya , Kutuliza unyevu na usafi wa binafsi , ustawi wa kijamii na kihemko na mifumo ya kiafya kutoka olimpiki maalum .


Wakati Noha Gab Allah, Mkurugenzi wa programu ya wachezaji mabingwa alisisitiza kuwa kila programu ya nchi zinazoshiriki iliwaita wachezaji  mabingwa wapya 3-5  kama siyo chini ya wachezaji 3 hadi wachezaji 5 , wanaotilia maanani kuhudhuria duru ya mafunzo kwa maisha ya kiafya na kuwakilisha wachezaji katika uwanja huo . Pamoja na kupeleka kwao mfumo wa maoni na hiyo ilikuwa hatua muhimu kwao kabla ya kushiriki katika duru .


Na kuhusu sifa za mchezaji bingwa , Noha aliongeza kusema kwamba umuhimu wa mchezaji asajiliwe katika olimpiki maalum ,  umri wake uwe angalau miaka 16 , anaweza kuelezea mawazo na maoni yake juu ya linalohusiana na olimpiki maalum na mambo mengine kwa jumla ,  anaweza kuongea hadharani , ana uhuru  , mzuri katika kuwasiliana na maingiliano ya kijamii , anatambua umuhimu wa programu ya kuamsha jukumu la wachezaji mabingwa - wawakilishi wa Afya - , anaweza kuandaa vidokezo na maoni  yake na kusikiliza vidokezo na maoni ya washiriki wengine , anaweza kufanya kazi katika kundi , anawakilisha wenzake wachezaji katika programu ya olimpiki maalum ya ndani , anafuatilia tabia za kiafya - anafanya mazoezi na anafuatilia ulinzi wa kiafya - na anatilia mkazo ili kuongeza maelezo yake katika uwanja huo, akilenga awe mfano bora kwa wengine  katika uwanja huo .


Ama kuhusu sifa za msindikizaji  , Fatuni anasema kuwa umri wake angalau unafikia miaka 25  , mjitoleaji au kocha au jaji au mwanachama mwenye Athari nzuri katika olimpiki maalum ya ndani tangu angalau miaka miwili, si mmoja wa familia ya mchezaji  , anamjua mchezaji bingwa mwanzoni , yupo tayari aendelee kuwasiliana na mchezaji bingwa wakati amhitaji ili kutekeleza  shughuli zinazo miongoni mwao programu ya olimpiki maalum , yupo tayari kumsaidia mchezaji  kuunda mawazo na mapendekezo yake , yupo tayari kutoa mazoezi ya ujuzi wa uongozi  kwa mchezaji bingwa mnamo angalau mwaka mmoja kuanzia duru ya mafunzo ianze  , vilevile, yupo tayari kushirikisha maoni yake ili kuendeleza programu ya wachezaji  mabingwa  na kuamsha jukumu lao la ndani  - haswa mchezaji bingwa  kama mwakilishi wa Afya .


Comments