Waziri wa Vijana akutana na wajitolea wa Kombe la Dunia la mikono katika Uwanja wa Kairo


Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alikutana , Ijumaa, katika ukumbi uliofunikwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo na kikundi cha vijana wa kujitolea katika kuandaa mashindano ya Mpira wa mikono ulimwenguni yatakayokaribishwa na Misri Januari ijayo kwa ushiriki wa timu 32 kutoka nchi tofauti za ulimwengu.



Waziri akasikilizia mkuu wa kamati ya kujitolea juu ya usambazaji wao kwa kumbi zote zilizofunikwa ambazo zimepangwa kukaribisha mashindano ya Kombe la Dunia kwa mpira wa mikono kwa upande wa vikundi vya sherehe na mapokezi, viwanja, ukumbi wa kuingia , malazi, uhamisho, kamati ya vyombo vya habari, kamati ya matibabu, na vikundi vingine.


Sobhy alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa vijana wanaojitolea katika kupanga mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni na kupata mafanikio kwa kuzingatia changamoto za kisasa za virusi vya Corona, akionesha wazi kazi ya maendeleo ya mkusanyiko wa kumbi zilizofunikwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo, na pia kuanzishwa kwa kumbi zilizofunikwa huko Borg Al Arab, mitaa ya sita Oktoba na mji mkuu mpya wa kiutawala.


Waziri huyo alisema kuwa ushiriki wa vijana wanaojitolea katika kuandaa Kombe la Dunia utaonesha picha ya ndani ya vijana wote wamisri, akiwatakia mafanikio katika kutekeleza michango yao na majukumu waliyoyapewa.


Alisema kuwa wajitolea katika Kombe la Dunia watafundishwa na wataalamu kadhaa kutoka Wizara ya Afya njia za kufuata utumiaji wa hatua za tahadhari na hatua za kuzuia virusi vipya vya Corona.

Comments