Waziri wa Michezo ashuhudia ufunguzi wa Olimpiki ya mikoa ya mpakani huko Sharm El-Sheikh


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alishuhudia sherehe ya ufunguzi  wa Olimpiki ya Mikoa ya mpakani, toleo la pili,  inayofanyika katika viwanja vya Jiji la Vijana na Michezo huko Sharm El-Sheikh,  inayofanyika kutoka siku ya 19 hadi 23 mwezi wa Desemba na inatekelezwa na Utawala mkuu wa Maendeleo ya Michezo kwa kuzingatia maslahi ya uongozi wa kisiasa Kwa kuendeleza mikoa ya mpakani na kufanya kazi ya kutumia nguvu za vijana wake.


Ufunguzi huo ulihudhuriwa na Meja Jenerali Khaled Fouda Gavana wa Sinai Kusini, Meja Jenerali Khaled Shuaib Gavana wa Marsa Matrouh, Meja Jenerali Muhammad Al-Zamalout Gavana wa Bonde Jipya na viongozi kadhaa wa Wizara ya Vijana na Michezo, wataalamu wa vyombo vya habari na viongozi kadhaa watendaji katika mikoa ya mpakani inayoshiriki.


Sherehe ya ufunguzi ilijumuisha utoaji wa maonyesho ya michezo kutoka Kitivo cha Elimu ya Michezo, Chuo Kikuu cha Aswan na Tala'a na vijana kutoka Wizara ya Vijana na Michezo.Mikoa ya Aswan, bonde jipya , Sinai Kaskazini, Sinai Kusini, Bahari nyekundu , Marsa Matrouh itashiriki kwenye Olimpiki.  Na hivyo katika mfumo wa Kutekeleza malengo ya kitaifa kwa kutoa programu na shughuli za michezo na pia kutoa huduma za michezo kwa sehemu zote za jamii ya Misri , haswa katika mikoa ya mpakani ili kuchangia kueneza tabia chanya kwa wachipukizi na vijana .


Olimpiki hufanyika kwa kushiriki michezo kadhaa, nayo ni, " Mchezo wa Khomasi ya Soka, mpira wa wavu, mpira wa wavu wa ufukweni, tenisi ya meza, mpira wa kasi wa karate, chesi, michezo ya nguvu, kuogelea" kwa wavulana na wasichana wa miaka 15 hadi 23, pamoja na mpira wa wavu kwa walemavu . Taa ya Olimpiki ulizinduliwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo mnamo Novemba 9 iliyopita.


Comments