Waziri wa Michezo ahudhuria mkutano wa waandishi wa habari wa kimataifa wa "Big Ramy" huko Piramidi
- 2020-12-28 13:31:07
Waziri wa Michezo alisisitiza kwa Big Ramy kujivunia na kuthamini mafanikio hayo makubwa aliyoyapata, pia yaliyomfanya hadithi ya ulimwengu wote mnamo siku chache zilizopita, akielezea kuwa mafanikio yake ni mwendelezo wa mfululizo wa mafanikio yaliyorekodiwa na michezo ya Misri kwa barua za mwanga katika mashindano yote ya Kiarabu, barani na kimataifa katika michezo tofauti.
Hiyo ilikuwa wakati wa mkutano wa waandishi wa habari wa kimataifa uliofanyika huko eneo la Piramidi, kwa kuratibiwa na Wizara ya Vijana na Michezo, kampuni ya mdhamini wa mchezaji na Shirikisho la Kujenga Mwili.
Dokta Ashraf Sobhy alimpongeza Bingwa wa Misri Big Ramy kwa kushinda lakabu ya Mr.Olympia, akisifu dhamira ya bingwa na uwezo wa kushinda, baada ya kupona kutoka Corona, na maandalizi bora ya mashindano, kuonesha mfano wa dhamira, changamoto na uwezo wa kufanikiwa.
Sobhy alisema: "Misri iliishi usiku mzuri sana, na vijana wote wanajivunia Big Rami, na bingwa huyo wa michezo hukamilisha picha ya bingwa anayependa nchi yake na hutoa picha bora ya michezo kuhusu Misri."
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri huyo aliashiria msaada kamili uliotolewa na serikali ya Misri chini ya uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi kwa wachezaji wote, na kuwahamasisha kuendelea na mafanikio yao na kutoa utendaji wao bora unaosimamia michezo ya Misri katika mashindano yote.
Big Ramy alisisitiza thamani ya mafanikio maishani mwa binadamu,na alitoa pongezi kwa hadhira bora ya kimisri ambapo alipata heshima na ukarimu mkubwa usio na mfano kutoka kwao.
Ramy alizungumzia mafanikio ya kihistoria, na maelezo yote ya kujiandaa kabla ya kusafiri kwenda Marekani, akiambukizwa na virusi vya Corona kabla ya mashindano na kutoa changamoto kwa hali hizo, kisha kujiandaa kwa mashindano hayo na kusafiri kwenda Marekani na pazia zingine na maelezo muhimu.
Islam Kartam, Mwenyekiti wa Taasisi ya Cosquad inayodhamini Big Ramy, alisema: "Ramy amegeuka akawa ishara kwa wanamichezo wachanga, kwani ana safari maalum iliyojaa mafanikio na shida ambazo alishinda mwishowe na kufikia ukumbi wa kutawazwa na kushinda ubingwa muhimu zaidi ulimwenguni mnamo wakati mgumu usio na nafasi ya kugombea kushinda kutokana na kuambukizwa na Corona na kumwache kando na mashindano yanayofikia Mr.Olimpya 2020.
Islam Kartam alisisitiza umuhimu wa kuunga mkono Wizara ya Michezo na jukumu lililochukuliwa na Dokta Ashraf Sobhiy, haswa kwa vile alikuwa akimfuata Ramy kila wakati, na alimwita kabla ya kusafiri kushiriki kwenye mashindano kumsaidia, na kuwa pamoja nawe na kumhakikishia kuwa kila mtu alimtarajia kupata mafanikio mapya kwa michezo ya Misri, ambayo ndio Ilikuwa na athari ya uchawi kwa mchezaji na ilimhamasisha katika awamu ngumu kama ile.
Comments