Waziri wa Michezo awapongeza klabu ya Al-Ahly kwa Tuzo ya Karne barani Afrika na inayotawazwa zaidi katika Mashariki ya Kati


Mahmoud Al-Khatib Rais wa Klabu ya Al-Ahly alipokea barua rasmi kutoka kwa Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Michezo; ili Kupongeza klabu ya Al-Ahly kwa kushinda tuzo ya "klabu ya karne barani Afrika na klabu inayotawazwa zaidi katika Mashariki ya Kati" kutoka kwa Shirika la  "Globe Soccer" .



Pongezi ya Waziri wa Michezo Dokta Ashraf Sobhy ilikuja katika mfumo wa msaada wa nchi, na Rais Abd El Fatah El-Sisi kwa klabu za Misri, zinazoongozwa na Klabu ya Al-Ahly;  ili Kuinua bendera ya Misri juu katika vikao vya kibara na kimataifa.


Al-Khatib Rais wa klabu hiyo alipokea tuzo ya "Globe Soccer" hapo jana kwenye sherehe kuu iliyofanyika huko Dubai, kwa kuhudhuria kwa viongozi wa Baraza la Michezo la Dubai, Gianni Infantino, Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, na Japo la mabingwa wa mpira ulimwenguni.


Mahmoud Al-Khatib alikuwa na shauku kubwa ya kushukuru Baraza la Dubai na mpango wa Shehe Mohammed bin Rashid Kwa sababu ya kujali kwake kwa mpira katika eneo la Kiarabu na ulimwengu wote, akisisitiza kuwa kuchagua Klabu ya Al-Ahly kuwepo kwenye hafla hiyo kama mwakilishi wa mpira wa miguu wa Kiafrika na Kiarabu ni heshima kubwa.


Ikumbukwe kwamba Shirika la "Globe Soccer"  lilizindua kura ya maoni tangu muda mfupi uliopita kwenye tovuti yake ili kuchagua klabu bora zaidi ulimwenguni na Mashariki ya Kati, ikiwa uamuzi wa kuchagua bora ni 60% kwa kamati ya wataalamu iliyoundwa na Shirika , na 40% ya uamuzi ni kwa maoni ya umma, na maoni ya walio wengi yameweka

kitambulisho cha tuzo hiyo

Katika kamati ya uteuzi , klabu ya Real Madrid ilishinda taji la Klabu ya Karne ulimwenguni, na Klabu ya Al-Ahly ilishinda taji la Klabu ya karne ya Afrika na mashindano inayotawazwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.


Comments