Waziri wa Vijana ahudhuria mkutano wa kufunga mashindano ya bora kwa mipango ya jamii
- 2020-12-31 16:43:13
Jumatatu jioni, Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia mkutano wa kufunga wa mashindano ya Bora kwa mipango ya jamii kwa msimu wa pili, ulioandaliwa na idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia katika wizara hiyo.
Shindano la Bora lilikuja kwa lengo la kusaidia vijana kushiriki katika mipango ndani ya jamii zao kuwasaidia uanzishaji wa mazingira mazuri ya maendeleo, ushirikiano na taasisi za asasi za kiraia, uanzishaji jukumu la vituo vya vijana, kuhamasisha vijana kwa ubunifu na uvumbuzi na mashindano yalizingatia kuwa mipango hiyo ihusiane na changamoto na shida kuu katika Jamii.
Mkutano huo ulijumuisha uwasilishaji wa mipango ya kushinda ya shindano ya bora kwa mwaka 2020, iliyoweza kupitisha hatua zote za mashindano kutoka tathmini na kushinda mashindano na mipango mingine na kati ya mipango iliyowasilishwa " Step to stop Cancer, Future zone, El Forsagia, Kenooz, Kalefni, Etgah, Business online, A walk for Archeology, Nefham Baad, Aeiz Atalim ."
Wamiliki wa mipango hiyo waliwasilisha malengo, maoni, dhamira ya kila mpango na mifumo yake utekelezaji kweli na msaada na mipango ya mafunzo inayostahili kutoka kwa Wizara ya vijana na michezo.
Dokta Ashraf Sobhy alisifu mipango iliyowasilishwa na maoni yao mazuri ya kuhudumia Jamii, akiashiria kutoka msaada kwa mipango hii na kuchangia katika utekelezwaji kweli , akitaka kutekelezwa kwa mashindano maalum ya mpango bora zaidi unaofikia idadi kubwa zaidi ya vijana kupitia mitandao ya kijamii na utumiaji wa njia za kiteknolojia.
Mwisho wa mkutano, Waziri huyo alitoa tuzo za mipango kumi iliyoshinda kwa mahudhurio ya Dina Fouad, mkuu wa Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia, Dokta Mervat Sayed Ahmed, Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Elimu ya kiraia na vijana viongozi, Youssef Wardani, Msaidizi wa Waziri na Mustafa Abdel Latif, mwakilishi wa Shirika la Eyouth mshiriki wa utekelezaji wa mashindano pamoja na Wizara ya vijana na michezo.
Comments