Kamati ya Wajitolea wa Mashindano ya Mpira wa Mikono Duniani yafuata mafunzo ya wajitolea katika ukumbi wa Borg Al Arab huko Aleskandaria


 Taarifa ya Wizara ya Vijana na Michezo inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo ilisema kwamba kamati ya Wajitolea ya toleo la 27 la Mashindano ya Mpira wa Mikono kwa Wanaume Duniani,  yatakayokaribishwa nchini Misri Januari hii, imefuatilia mafunzo ya mwisho ya wajitolea katika ukumbi wa Borg Al Arab huko Aleskandaria.


 Kamati ilitazama mazoezi ya mwisho katika ukumbi mkuu, viingilio vyake na kutoka, eneo la VIP, malango, na stendi, huku kukiwa na hatua kali za tahadhari.


 Mafunzo ya mwisho yalifanywa mbele ya idadi kadhaa ya kamati  ya kujitolea ya ubingwa, Bi.Nagwa Salah,  Katibu wa Wizara, Mkuu wa Utawala wa Kati wa Programu za Utamaduni na Hiari kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, Dokta. Sharif Abu Al-Enein, na Bw.Islam Abdel Aziz.


 Ikumbukwe kuwa mashindano hayo yatakaribishwa  kutoka Januari 13-31 kwenye kumbi za Uwanja wa Kairo, mji mkuu wa kiutawala, Oktoba 6, na Borg Al Arab huko Aleskandaria.


Comments