Ashraf Sobhy : " Maisha Mema " yaelekea nguvu za jamii kwa kuhudumia vijana wa Misri
- 2021-01-07 11:42:42
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo alishuhudia kuzindua Wizara ya wafanyakazi iliyo kwa uongozi wa Dokta Muhammed Safan kwa awamu ya nne ya mpango wa " Maisha Mema " ili kurejesha upya na kufanyia kazi vitengo vya mafunzo vya rununu 14 vijijini na vitongojini vidogo vya mikoa mbalimbali.
Hivyo ilikuja kwa mahudhurio kamanda " Kaml El-waziri " Waziri wa usafirishaji , Dokta" Neven El- Qubqk" Waziri wa mshikamano wa kijamii , " Osama Haikal " Waziri wa nchi wa vyombo vya habari , kamanda " Khaled Abdelall " Gavana wa mkoa wa Kairo , " El-Gbali Maraghi " Mkuu wa Shirikisho kuu la taasisi ya wafanyakazi wa Misri , " Irik Oshlan " Mkurugenzi wa ofisi ya Shirika la kazi la kimataifa , " Mungstab Hayali " Mkurugenzi wa mfumo wa chakula wa ulimwengu, Jopo la waheshimiwa wa nchi na wanachama wa baraza la wawakilishi na wazee katika sherehe kubwa kwenye uwanja wa michezo wa Kairo wa kimataifa .
Awamu ya nne ya kurejesha upya na kufanyia kazi vitengo vipya vya mafunzo vya rununu 14 vijijini na vitongojini vidogo vya mikoa ya Giza " kijiji cha Manshit El- Qanatr " , Port Said " Mtaa wa Elzuhur " , bahari nyekundu " Garda" , Gharbia " El-mahala " El-munufia " mji wa El-shuhadaa " , El-sharkia " El-smakin kituo cha Al-hussaina " Bani Suif " kijiji cha El-harga " , Dumiat " Abu Rashid " , Ismalia " Tal El- kbir " , Sinai Kusini " wady bdur sina " pamoja na mikoa 4 mingine, ambapo huainisha vijijini vinavyohitaji zaidi misaada .
Sobhy kupitia uzinduzi wa mpango alisisitiza kwamba mpango wa Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri unalenga kuelekeza nguvu za jamii zote ili kuhudumia vijana wa Misri katika viwango mbalimbali vya mipango au elimu au michezo au kikazi .
Waziri huyo aliashiria kuwa mpango wa Maisha Mema unarahisisha mustakabali kwa vijana , akiongoza kusema kwamba vituo vya vijana wa Misri vinakaribisha vijana wake katika mpango wa Maisha Mema kwenye mikoa yote ya Jamhuri .
Mawaziri walichunguza vitengo vya mafunzo vya rununu , wakisifu juhudi za Wizara katika kuimarisha na kuendeleza vitengo vile mpaka vikuwa jinsi vilivyo ili kutosheleza kazi za uundaji mavazi , ushonaji , mabomba , Afya na umeme ya nyumba , wakiuliza juu ya masaa ya mafunzo , idadi ya wanafunzi katika kila kitengo na orodha ya kusubiri inayohusika wanaofundishwa katika mikoa yote na kiwango cha mahitaji ya kupata mafunzo ndani yake .
Comments