Waziri wa Michezo ahudhuria mechi ya kirafiki ya timu ya taifa ya mpira wa mikono ya Misri mbele ya Japan


 Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia mechi ya timu ya taifa ya mpira wa mikono ya Misri na mwenzake wa Japan, iliyofanyika katika ukumbi uliofunikwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Kairo, kama sehemu ya maandalizi ya timu hiyo ya Misri kushindana kwenye Mashindano ya Dunia, ambayo Misri inaandaa kutoka Januari 13 hadi 31, kwa ushiriki wa nchi 32  ulimwenguni kote.



 Waziri huyo alithibitisha kuwa mechi hiyo ilishuhudia utekelezaji madhubuti na sahihi kwa hatua zote za tahadhari na mpango wa matibabu kulingana na mfano wa bubble ya matibabu iliyoanzishwa kwa timu, vifaa vya kiufundi na kiutawala zinazoshiriki katika Kombe la Dunia.


 Kabla ya mechi hiyo, Sobhy alishuhudia utendaji wa kamati ya kujitolea na njia za kuingia na kutoka kwa raia, ambazo zimepangwa kwa 20% ya uwezo wa kila ukumbi.Waziri wa Vijana na Michezo alisifu taratibu zinazofuatiliwa na wajitolea katika kushughulikia mechi hiyo kama mfano wa mechi za mashindano,  itakayoanza mnamo siku chache.


 Sobhy ameongeza kuwa mashindano ya mpira wa Mikono ulimwenguni huko Misri ni mwendelezo wa mwenendo wa maendeleo wa Misri wakati wa enzi ya Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, akiashiria kuwa jimbo la Misri limeandaa kumbi za ubingwa na kumbi za mafunzo kwa kiwango cha juu na kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.


 Sobhy alitoa wito kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Misri kufanya bidii mnamo kipindi kijacho na wakati wa mashindano kufikia msimamo unaofaa nafasi ya Misri katika ngazi zote.


 Ikumbukwe kuwa Kombe la Dunia la mpira wa mikono nchini Misri litafanyika katika kumbi 4, nazo ni ukumbi uliofunikwa katika uwanja wa kimataifa wa Kairo, uwanja wa mji kuu wa Utawala, ukumbi wa Borg Al Arab huko Aleskandaria, na ukumbi wa 6 Oktoba.

Comments