Vituo vya vijana vya Aleskandaria vyapambwa kwa mabango ya kukaribisha kombe la dunia


Vituo  kadhaa vya vijana  huko mkoa wa Aleskandaria  vimetilia mkazo kupandisha mabango na bendera za nchi kwa ajili ya kuonesha ukaribu kwa nchi zinazoshiriki katika michuano ya dunia ya mpira wa mikono na miongoni mwao ni vituo  vya vijana wa El-haramain , El-shalalat, Borg Al-arb alkadem , Abu Qer , Hars , Al-amiria na vinginevyo vya vituo vya Aleskandaria.


Kwa upande wake , Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba  ukaribisho wa Misri kwa  michuano ya dunia kwa mpira wa mikono hauzingatiwi tukio kubwa la michezo tu bali unazingatiwa  maendeleo  makubwa na kuwepo kwa jamii ya Misri  katika nyanja  zote za kiuchumi, kiutalii , kijamii na kiutamaduni , pamoja na mabadiliko ya ujenzi katika miundombinu ya michezo  ambayo michuano ilikuwa ndiyo sababu ya kuifanikisha kwa mtindo wa kiulimwengu  na mnamo wakati huu  .


Aliashiria kuwa misaada ya ukaribisho wa Misri kwa tukio hilo  inayotolewa na Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri hauna kiasi ,  

Inazingatiwa jiwe la kimsingi katika mafanikio yote yanayohusiana na maandalizi ya michuano na ambayo yametekelezwa mnamo kipindi kisichozidi miaka miwili tu  ima katika ujenzi unaohusu kumbi za michuano au katika awamu za mchakato wa maandalizi kwa michuano . 


Bibi harusi wa bahari nyeupe ya kati (Aleskandaria) inakaribisha mashindano ya timu za Kroatia , Qatar , Angola , Japan , Slovenia , Urusi , Belarusi na Korea.

Comments