Mmisri na Mwafrika wa kwanza yupo kati ya wachezaji 100 bora ulimwenguni katika Chesi

Mmisri  na Mwafrika wa kwanza yupo kati ya wachezaji 100 bora ulimwenguni katika Chesi

 

Mmisri Basem Amin aliacha Utabibu kujishughulisha Chesi


Hadithi ya shujaa mashuhuri ambaye aliheshimu Chesi ya Misri katika vikao vya kimataifa na kuifikisha nchi yake kuelekea awamu ya kimataifa.


Shujaa huyo mbele yenu, ndiye Mmisri wa kwanza, Mwarabu na Mwafrika kushinda taji la Super Grand Master, ambalo linachukuliwa kama kiwango cha juu cha Chesi,


Mchezaji Mmisri, Mwarabu,na Mwafrika wa kwanza kushiriki katika wachezaji 100 bora duniani wa Chesi.


Alicheza mbele ya anayeainishwa namba ya kwanza ulimwenguni, na aliweza kuapta sera naye na kisha akamshinda Nakmura, mwenye namba ya pili wa Marekani na kuwashinda wakubwa wa  mchezo hadi akafikia kiwango cha 41 ulimwenguni.


Alikataa uraia kwa Marekani na akaamua kuiwakilisha Misri, kwa ada ndogo sana, hata ukitaka sema kwa bila mshahara kabisa!


 Yeye husafiri kila wakati kwenye mashindano kwa gharama zake za kibinafsi kubeba bendera ya nchi yake kati ya majitu wakubwa wa mchezo. Yeye ndiye Daktari Mpasuaji Basem Amin, Bingwa wa Misri na Afrika katika mchezo wa Chesi!

Comments