Timu ya taifa ya mpira wa mikono ya Japan yatembelea eneo la Piramidi


Eneo la makaburi ya Piramidi lilikuwa mwenyeji wa timu ya taifa ya mpira wa mikono ya Japan, itakayoshiriki katika toleo la 27 la Mashindano ya Dunia ya Wanaume ya 2021, Misri itakuwa mwenyeji kutoka Januari 13 hadi Januari 31. 


Ziara hiyo inakuja ndani ya muktadha  wa ushiriki wa Wizara za Utalii na  Mambo ya kale katika mashindano hayo kwa kuwasilisha mipango na vifaa vya Utalii kwa timu za taifa zinazoshiriki mashindano hayo na kwa umati wa mashabiki watakaohudhuria kutoka nje ya nchi kuzipa moyo timu zao.


Wakati wa kuwepo kwao huko Kairo kushiriki kwenye mashindano, timu ya taifa ya  Japan ilikuwa na hamu ya kutembelea Piramidi, Sphinx na Panorama, pamoja na kuzingatia hatua yza tahadhari na udhibiti wa Usalama wa Afya uliowekwa kutoka kwa  Shirikisho la mpira wa mikono la kimataifa kwa wanachama wa timu zinazoshiriki na zile za kutembelea maeneo ya akiolojia na majumba ya kumbukumbu huko Misri.


Ikumbukwe kwamba timu hiyo ya Japan ndiyo timu ya kwanza inayoshiriki kwenye mashindano kufikia Kairo.


Comments