Waziri Mkuukuu : Tunafanya juhudi zote kutokea michuano ya mpira wa mikono kwa sura inayoshangaza Dunia
- 2021-01-12 12:20:30
Mustafa Madboli , Waziri Mkuu, Jumapili jioni,aliongoza mkutano wa kamati ya juu kwa michuano ya Dunia kwa mpira wa mikono kwa wanaume 2021; ili kufuatilia mipango ya mwisho ili kuzindua michuano mnamo terehe 13 Januari hii .
Pia Khaled Elanani , Waziri wa Utalii na vitu vya kale ,Mohamed Maait , Waziri wa fedha ,Mahmoud Twafiq , Waziri wa mambo ya ndani ,Hala Zayed , Waziri wa Afya na Makazi ,Mohamed Manar Enapa , Waziri wa Usafirishaji wa ndege, wahusika wa mashirika yanayohusika , walishiriki katika mkutano kupitia video conference ,pia Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo ,Dokta Hassan Mustafa , Mwenyekiti wa Shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono ,Hussein Labib , Mkurgunzi wa michuano ,Hesham Nasr , Mwenyekiti wa Shirikisho la kimisri kwa mpira wa mikono walihudhuria katika makao makuu ya baraza la mawaziri .
Waziri Mkuu alianza mkutano ,kwa kufanya upya kwa umuhimu wa kufanya juhudi ili kutokea mashindano hayo kwa njia inayoshangaza Dunia , akiashiria dharura kali juu ya kulazimisha kwa hatua zote za kitahadhari na kinga ili kujikinga kutoka kwa Virusi vya Corona ,na kutozembea kuzitumia kwa nguvu ,ili kuhifadhi washirki wote katika tukio hilo muhimu la kimchezo .
Aliashiria kuwa Rais Abd El Fatah El-Sisi anafuatilia maelezo ya taratibu na maandalizi kwa mashindano moja kwa moja,aliamuru kwa kuchukuliwa hatua zote za kinga ,na kufanya kazi kwa mashindano hayo kwa njia ya ustaarabu .
Wakati Ashraf Sobhy , Waziri wa vijana na michezo alieleza, kuwa timu zitaanza kufikia kuanzia kesho Jumatatu , akiashiria taratibu zinazoendelea pamoja na Wizara zote na mashirika yanayohusika kwa upande wa linalohusiana na mipango na mingine .
Kwa upande wake ,Hassan Mustafa , Mwenyekiti wa Shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono ,alitoa shukrani juu ya juhudi zinazofanywa ili kufanikisha michuano ile .
Wakati wa mkutano huo ,imeshakubaliwa mechi zote za michuano zitakuwa bila ya mashabiki ,miongoni mwa hatua za kitahadhari zinazochukuliwa kwa nchi ili kupambana na Virusi vya Corona ,na mahudhurio yatakuwa kwa watangazaji wa vyombo vya habari, na idadi fulani ya mialiko na mahitaji ya Shirikisho la kimataifa .
Wakati wa mkutano huo ,taratibu za kiafya na kinga zikifuatiliwa,taratibu za kupokea kwa jumbe za kimichezo ,taratibu za bima ,upangaji wa mchakato wa kuingia na kutoka kwa timu za kimichezo zinazoshiriki katika michuano ,na mazoezi yatakayofanywa kwao.
Comments