Waziri wa michezo na Mkuu wa Taasisi ya uhandisi wakagua mkusanyiko wa kumbi za Hassan Mostafa
- 2021-01-14 11:46:47
Dokta " Ashraf Sobhy" Waziri wa vijana na michezo na Kamanda Jenerali "Ihab El-far " Mkuu wa Taasisi ya uhandisi Jumanne, walikagua mkusanyiko wa kumbi za Hassan Mostafa katika eneo la sita Oktoba , katika mfumo wa maandalizi ya kukaribisha michuano ya dunia ya mpira wa mikono wa Misri 2021 , inayopokea mashindano ya makundi ya kwanza na tano .
Mkusanyiko wa Hassan Mostfa huko sita Oktoba unakaribisha mashindano ya makundi mawili :- la kwanza na la tano .
Kundi la kwanza linajumuisha :- Ujerumani - Hungary- Uruguay - Ras Alakhdr
Kundi la tano :- Norway - Austria -Ufaransa - Marekani .
Hivyo inakuja katika mfumo wa ziara za uchunguzi zinazofanywa na Dokta Ashrf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo , leo, kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya mwisho ili kukaribisha Misri kwa michuano ya Dunia ya mpira wa mikono itakayozinduliwa kesho na itaendelea hadi tarehe 31 Januari hii .
Waziri huyo alisisitiza kwamba uongozi wa kisiasa unatoa njia za misaada kadha kwa michuano ili kutoa kwa sura nzuri na inayofaa kwa jina na hadhi ya Misri Duniani katika kuandaa matukio na michuano ya kimataifa .
Sobhy aliashiria kuwa kumbi zinazokaribisha michuano zinazingatiwa kuwa viwanja vya michezo vikubwa vinavyoonesha nafasi ya nchi ya Misri kwenye vyeo vya juu zaidi sawa kwa kupokea matukio na michuano ya michezo tofauti ya kimataifa au kutoa miundombinu ya michezo ya kimataifa kwa timu za taifa za Misri, linaloxiwezesha kufikia mafanikio ya michezo katika mashindano tofauti ya bara , kimataifa na kiolimpiki.
Waziri huyo, Asubuhi ya leo alikagua ukumbi unaofunikwa katika mji mkuu wa kiutawala ili kufuatilia maandalizi ya mwisho kabla ya kuzindua michuano .
Comments