Misri yashinda Chile (35-29)


Timu ya taifa  ya mpira wa mikono ya Misri ilifungua Kombe la Dunia kwa kushinda timu  ya Chile kwa matokeo  (35-29), katika toleo lake la 27, lililofanyika huko Misri mnamo Januari 13-31.


Rais Abd El Fatah El-Sisi alihudhuria sherehe ya ufunguzi wa mashindano hayo, akisema: "Kwa Jina la Mwenyezi Mungu na kwa baraka ya Mwenyezi Mungu, tunatangaza ufunguzi wa Mashindano ya 27 ya Wanaume kwa Mpira wa Mikono Duniani kwenye Jamhuri ya Kiarabu ya Misri."


Timu ya taifa ya Misri inakabiliwa kwa changamoto kubwa wakati wa Kombe la Dunia, kama inavyoonekana kwa mara ya 16 katika historia yake katika mashindano ya ulimwengu, na ni mara ya pili mashindano hayo kufanyika nyumbani baada ya toleo la 1999 ambapo "Mafarao" walishika nafasi ya saba.

Comments