Waziri wa Michezo ahudhuria mechi ya Denmark na kongo ya Demokrasia


 Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Doota Hassan Mostafa, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa mikono, walishuhudia ukumbi uliofunikwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo;  Mechi kati ya Denmark na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ndani ya Mashindano ya Kundi la nne Duniani kwa Mpira wa Mikono, yanayokaribishwa kwa Misri mnamo Januari hii.


 Timu ya taifa ya Denmark ilishinda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa alama 39/19 katika mechi  iliyoshuhudia uongozi wa timu ya Denmark, bingwa wa ulimwengu, shukrani kwa uzoefu wa wachezaji wake, baada ya Denmark kupata 23/10 katika kipindi cha kwanza kwenye Kombe la Dunia la Mikono.


 Timu hizo mbili zinacheza katika kundi la nne linaloshiriki katika ukumbi mkuu wa Uwanja wa Kimataifa wa Kairo, ambao pia ulishuhudia timu ya Argentina ikipata ushindi mgumu dhidi ya timu ya Bahrain kwa alama 24-21, mbele ya Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy na Dokta Hassan Mustafa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikomo la Kimataifa, Balozi wa Bahraini na Katibu wa ubalozi wa Argentina  .


 Katika raundi ifuatayo ya Kundi la nne,  Argentina na Congo zitacheza pamoja, wakati Bahrain itakutana na Denmark.

Comments