Mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania asifu uratibu wa kimisri kwa kombe la dunia la mpira wa mikono
- 2021-01-20 11:09:42
Raul interrius , Mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania na mchezaji wa klabu ya Barcelona ya kihispania alisifu uratibu wa kimisri kwa toleo la 27 kwa kombe la dunia la mpira wa mikono.
interrius alisisitiza kwamba mashindano ya dunia nchini Misri yanashuhudia uratibu bora na mkubwa unaofaa historia ya mpira wa mikono ulimwenguni na timu ya kitaifa ya nchi yake inajisikia furaha kwa kuwepo kwake nchini Misri na kugombea katika kombe la dunia.
Na interrius alisema : "Misri inapanga mashindano kwa njia nzuri na kubwa katika hali hizo ngumu kwa sababu ya virusi vya Corona
Na aliongeza : " Naipongeza Misri kwa ajili ya uratibu mzuri huo na taratibu zote za tahadhari za kipekee zinazochukuliwa ili kuwalinda wote "
Na aliendelea : "Taratibu ni nzuri na zimepangwa vizuri na kuna ufahamu mkubwa katika ya wapangaji wote ili kutimiza mashindano kwa njia nzuri "
Alihitimisha: "Ushiriki wa timu 32 kwa mara ya kwanza unaongeza nguvu na msisimko kwa mashindano hayo, tuko kwenye njia sahihi, tulifunga sare na Brazil baada ya kucheza kwa nguvu kwenye mechi ngumu, kisha tukaishinda Poland, na tunatafutia kushinda mechi inayofuata ili kufikia raundi inayofuata na tutaendelea kutoa kiwango bora kabisa ili kuwafurahisha mashabiki wa nchi yetu.
Uhispania inaongoza Kundi la Pili kwa Kombe la Dunia, baada ya mechi mbili, kwa kupata alama tatu kutoka sare dhidi ya Brazil na ushindi dhidi ya Poland.
Comments