Ashraf Sobhy anapokea rais wa Shirikisho la kiafrika kwa Mieleka

 Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, anapokea Fouad Muskout, Rais wa Shirikisho la kiafrika kwa Mieleka na mwanachama wa Shirikisho la Kimataifa, kwa mahudhurio ya Jenerali  Ahmed Nasser, Rais wa Shirikisho la kiafrika (UCSA) na Issam Mohamed Ismail, Rais wa Shirikisho  la kimisri kwa Mieleka .

 

Mkutano ulijadili maendeleo ya mchezo wa Mieleka pamoja na utoaji wa msaada kamili kwa shirikisho, pamoja na kupanua msingi wa mazoezi ya Mieleka na mashindano ya kimichezo nchini Misri na Afrika.

Rais wa Shirikisho la kiafrika alisifu uratibu wa ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Shirikisho la kimisri kwa Mieleka  kwa upande  mmoja na kati ya wizara na Shirikisho la kiafrika kwa Mieleka kwa upande mwingine.

Waziri wa Vijana na Michezo alimshukuru Mheshimiwa Fouad Muskout kwa  msaada wake kwa Shirikisho la kimisri kwa Mieleka.

Kwa upande mwingine, Fouad Meskout alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa kukaribisha kwake kwa joto, akisisitiza kwamba Misri ni nchi yenye historia  kubwa na ndefu ya kimichezo hasa katika mchezo wa Mieleka na pia alimsifu uwezo wa Misri kwa kuandaa na kukaribisha kwa michuano ya kimichezo kwenye ardhi  yake.

Comments