Waziri wa Michezo ahudhuria mechi ya Brazil na Hungary kwenye Ukumbi wa michezo huko mji mkuu wa kiutawala
- 2021-01-24 12:48:50
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, pomoja na Dokta Hassan Mostafa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono la kimataifa, walishuhudia mechi ya Brazil na Hungary katika raundi kuu kwa kundi la kwanza kwenye ukumbi wa mazoezi katika mji mkuu mpya wa kiutawala.
Pia, mechi hiyo ilihudhuriwa na Balozi wa Brazil "H.E.Antonia de Aguiar Patriote" na mkewe Bi. "Tania Cooper Patroiote" na Balozi wa Hungary "H.E.Andras Kovacs" na mtoto wake "Bence Kovacs".
Timu ya kitaifa ya Hungary iliishinda mwenzake wa Brazil kwa 29-23 kwenye kundi la kwanza, iliyozinduliwa katika ukumbi wa michezo katika mji mkuu wa kiutawala kama sehemu ya mashindano makuu ya raundi ya Kombe la Dunia la Mikono la Wanaume la Misri la 2021.
Kabla ya kuhudhuria mechi hiyo, Waziri wa michezo na Rais wa Shirikisho la Mikono la kimataifa walifuatilia utekelezaji wa hatua za tahadhari, kinga na udhibiti katika ukumbi wa mazoezi katika mji mkuu mpya wa kiutawala.
Na kuhudhuria kwa Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, kwa mechi hiyo ni sehemu ya ufuatiliaji wake wa kila siku wa shughuli za Mashindano ya Mikono ya Dunia ya Misri 2021, Misri itakayokuwa mwenyeji mnamo kipindi cha Januari 13-31 kwa ushiriki wa timu 32.
Ikumbukwe kwamba timu ya Brazil na timu ya Hungary zimo ndani ya kundi la kwanza, linalojumuisha Uhispania, Ujerumani, Poland na Uruguay.
Comments