Waziri wa Michezo afanya mkutano wake wa pili na wakuu wa jumbe zinazoshiriki katika mashindano ya mpira wa mikono Ulimwenguni


Katika muktadha wa mikutano yake na wakuu wa ujumbe ulioshiriki katika mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni, yanayoandaliwa kwa Misri kutoka 13 hadi 31 Januari 2021, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alifanya mkutano kupitia (Video Conference) na wakuu wa jumbe zilizoshiriki mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni kuwahakikishia taratibu za kiafya zinazofuatwa na taratibu. Inahitajika kuhifadhi washiriki wote kwenye Kombe la Dunia, kwa mahudhurio ya Dokta Hassan Mostafa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono la kimataifa, Mhandisi Hisham Nasr, Mwenyekiti wa kamati iandaayo kombe la Dunia na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono la Misri, Kocha Hussein Labib, Mkurugenzi wa toleo la 27 la mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni kwa wanaume" Misri 2021 " na Dokta Alaa Eid, Mkuu  wa kamati ya matibabu.


Mkutano huo ulijumuisha kujadili maswali yote kutoka kwa wajumbe juu ya maendeleo ya taratibu na udhibiti wote wa kiafya, uliotumiwa katika mashindano hayo, wakati wa mkutano huo, Dokta Ashraf Sobhy, wayziri wa Vijana na Michezo, alithibitisha maendeleo wa utekelezaji wa hatua za tahadhari za kiafya kwa wajumbe na timu zilizoshiriki kabisa bila kasoro lolote, akionesha ufuatiliaji wake wa kila siku kwa kumbi zote za kukaribisha mashindano ya kombe la Dunia, hoteli za malazi na maelezo yote ya mchakato wa shirika kuangalia washiriki wote kutoka nchi tofauti za ulimwengu.


Na Sobhy alielezea Shukrani zake kwa mfumo wa matibabu wa Misri na wanachama wote wa wafanyakazi wa matabibu na kamati kulingana na shirika na kiwango cha kujitolea kwao na uzalendo, haswa kwa kuzingatia utekelezaji wa hatua za tahadhari zilizowekwa kwa wajumbe na timu zinazoshiriki, Waziri wa Vijana na Michezo ameongeza kuwa uratibu unaendelea kila saa kati ya Wizara ya vijana na michezo, Wizara ya afya na wakazi, na wizara  zote husika, wakala na taasisi.


Kwa upande wake, Dokta Hassan Mostafa alisema kuwa hatua za kiafya na tahadhari katika mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni zinawakilishwa mfano wa kipekee uliotokana na juhudi kubwa na uratibu wa kudumu kati ya Mamlaka zote zinazohusika, kwenye mbele wa wizara ya vijana na michezo na kamati iandaayo inayoongozwa na Mhandisi Hisham Nasr na Kocha Hussein Labib, Mkurugenzi wa mashindano hayo, akisifu hatua hizo zitakazokuwa mfano kwa kiwango kwa kuzingatia changamoto ya virusi vipya vya Corona.


Mwenyekiti wa kamati iandaayo, Mhandisi Hisham Nasr, alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa msaada wake kamili kwa mashindano hayo, akibainisha kuwa mambo ya shirika kwenye mashindano yanatumika kwa taaluma isiyo ya kawaida.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa mashindano hayo, Kocha Hussein Labib, alielezea mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni huko Misri ni mashindano ya kihistoria yaliyofanyika nchini Misri katika nyanja zote za kupanga, matibabu na kiufundi.


Pia, mkutano huo ulihusu njia za kushughulikia kesi zozote zinazothibitisha kuwa na changa kwa uchunguzi wao wa kimatibabu kwa Corona, kesi hizi ziligawanywa katika kesi rahisi na zitatengewa katika moja ya hoteli zilizotengwa kwa ajili ya kutenganisha kesi chanya za magonjwa na katika hali zingine zinazohitaji huduma kubwa matibabu, watahamishiwa kwa moja ya hospitali maalum za Wizara ya afya ya Misri kukamilisha huduma zao za afya baada ya kufanya uchambuzi na miale inayohitajika.


Pia, mkutano ulishughulikia kujibu maswali yote yaliyowasilishwa na wakuu wa ujumbe kuhusu udhibiti wa afya na itifaki za matibabu zitazotumika kwa wachezaji ikiwa kuna kesi chanya pamoja na zile ambazo hufanywa kila siku kwa washiriki, ambapo matokeo yao yataotangazwa na kutumwa siku hiyo kwa washiriki wote.


Mwishoni mwa mkutano, wakuu wa wajumbe walioshiriki walisifu hatua za tahadhari zilizochukuliwa ndani ya mashindano hayo, utangulizi kwa serikali ya Misri juu ya mpangilio mzuri, wakigundua kuwa serikali ya Misri inachukua njia mpya katika kuandaa mashindano ya kimataifa kwa kuzingatia hofu ya ulimwengu ya athari za Corona.


Katika muktadha unaofanana, Waziri wa Vijana na Michezo alifanya mkutano wake wa mara kwa mara na mameneja wa kumbi zinazokaribisha Kombe la Dunia kupitia mkutano wa video Conference, mkutano huo ulishughulikia msisitizo juu ya udhibiti na taratibu zote zilizowekwa kwa mpango wa matibabu unaotumika kwa umakini.


Wakurugenzi wa kumbi wakisisitiza kwamba mambo yote ya hatua za tahadhari ndani ya kumbi zinaendelea kwa kasi hadi wakati wa mwisho wa kuhifadhi wajumbe na timu zinazoshiriki mashindano hayo.


Comments