Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo, alisifu utendaji bora wa wachezaji wa timu ya kitaifa mpira wa mikono katika mechi yao dhidi ya timu ya kitaifa ya Slovenia katika raundi ya mwisho ya kundi la nne, kwenye duru kuu ya mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni huko Misri.
Waziri huyo aliipongeza timu ya kitaifa ya mpira wa mikono baada ya sera 25-25 pamoja na Slovenia, kufikia robo fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kutoa utendaji bora katika mechi hiyo na kurudi tena baada ya kupoteza kwa mabao manne katika kipindi cha kwanza,ili kufunga sare katika mechi hiyo na kufikia pamoja na nukta saba kwa robo fainali.
Dokta Ashraf Sobhy alithibitisha kuwa mahudhurio ya Waziri Mkuu Mostafa Madbouly kwa mechi ya leo kati ya Misri na Slovenia ni ujumbe unaothibitisha uungaji mkono wa serikali katika taasisi zake zote kwa timu ya Misri katika hatua tofauti za mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni.
Ikumbukwe kuwa Misri inakaribisha mashindano ya mpira wa mikono Duniani 2021, kwa ushiriki wa timu 32 na hiyo ni mnamo kipindi cha Januari 13-31.
Comments