Waziri wa Michezo ajadili pamoja na Shirikisho la Mpira wa Kikapu kueneza mchezo huo shuleni
- 2021-02-20 20:29:32
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, amekutana na Magdy Abu Farikha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri, na Dokta Eman Hassan, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo la Shule ya Misri, kujadili mifumo ya kueneza mpira wa kikapu shuleni.
Waziri huyo alisisitiza kwamba uongozi wa kisiasa unatoa Umuhimu mkubwa kwa michezo na unaielezea kama Usalama wa kitaifa, ambayo imeonesha zaidi ya mara moja umuhimu wa kufanya mazoezi ya michezo na utunzaji wa upande wa afya ya vijana, kukuza uwezo wa akili na ukuaji wa mwili, na kuzingatia kuwepo kwa michezo katika shule na vyuo vikuu anuwai.
"Sobhy" alielezea matarajio yake ya kueneza michezo shuleni kupitia Ushirikiano pamoja na Wizara ya Malezi na Elimu na Elimu ya kifundi, ili kutoa vizazi wapya wanaooendesha michezo kwa aina zake zote, na anasisitiza jukumu la Wizara ya Vijana na Michezo katika kueneza utamaduni wa michezo shuleni.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Dokta Amr Haddad, Msaidizi wa Waziri wa Maendeleo ya Michezo, Dokta Muhammad Al-Kurdi, Dokta Abdul-Awal Muhammad, Msaidizi wa Waziri wa Utendaji wa Michezo, Dokta Sonia Abdel-Wahab, Mkuu wa Idara kuu ya Wizara kwa Maendeleo ya Michezo. , Dokta Ghada Jamal El-Din, Mkurugenzi Mkuu wa Idara kuu ya vikundi maarufu, na Mahmoud Abdel Aziz, Mkurugenzi Mkuu wa Utawala wa Umma kwa mashirikisho maalum na kamati za michezo kwenye Wizara hiyo.
Pia Waziri wa Vijana na Michezo alikuwa akikutana na Mhandisi Hisham Nasr, Rais wa Shirikisho la Mpira wa mikono la Misri, kujadili njia za kueneza mpira wa mikono shuleni.
Comments