Waziri wa Kilimo anawapokea vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika katika kituo cha tafiti za Kilimo na anaonyesha nyanja za ushirikiano wa pamoja na bara la kiafrika kwa kuhakikisha maendeleo

Dokta Ezz Eldin Abo Stet "Waziri wa Kilimo na kurekebisha ardhi " aliwapokea vijana waafrika wanaoshiriki katika Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika ", kwenye kituo cha Tafiti za Kilimo na hayo mnamo matukio ya Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika " uliotolewa kwa Wizara ( Ofisi ya vijana waafrika, na Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia) chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuly "Waziri mkuu", mnamo kipindi cha 8 hadi 22 Juni 2019, kwa kushirikiana na Shirikisho la vijana waafrika.


Na mkutano huu ulihudhuriwa, Dokta Muhamed Solaiman "Rais wa kituo cha tafiti za Kilimo" na Dokta Naeem Meselhy"Rais wa kituo cha tafiti za Jangwa, na Dokta Sherin Asem "Naibu wa kituo cha tafiti za Kilimo".


Na mnamo mkutano huu waziri wa Kilimo alisisitiza juu ya shime ya nchi ya kimisri kwa Uongozi wa "Abd Elfatah Elsisi " ya kushirikiana na bara la kiafrika, akiashiria kwa mtazamo na mkakati wa Misri katika kutumika Rasilimali zote na za binadamu pia zinazopatikana barani mwa Afrika ili kuhakikisha maendeleo endelevu.


Pia bwana Abu Setet alionyesha juhudi za kimisri na ushirikiano wa pamoja na bara la kiafrika katika uwanja wa Kilimo kwa njia inayoelekea na mielekeo ya Umoja wa kiafrika, akiashiria kwa mashamba ya kimisri barani Afrika, yanayokadiria kwa mashamba manane na yanafanya kazi za kimafunzo na kiongoza, na inayotarajiwa kuyaongeza kwa mashamba 22 kwa kumaliza mwaka wa 2020.


Na bwana Abu Setet alifafanua kwamba uhusiano wa Misri na Afrika ulipatikana tangu Rais aliyekufa Gamal Abd Elnasser mnamo kilele cha kiafrika cha kwanza kilichofanyikiwa katika Adis Ababa mwaka wa 1963, akiashiria kwa harakati za Ukombozi zilizoongozwa na Abd Elnasser kwa kiwango cha kisiasa barani Afrika, linalosababisha maendeleo na ushirikiano mwenye faida pamoja na bara la kiafrika khasa Kilimo inazingatiwa nguzo kuu katika maendeleo ya mahusiano kati ya nchi.


Na Waziri aliashiria kwamba Uzalishaji wa Kilimo unazingatiwa mhimili mkuu kwa nchi za kiafrika, alisisitiza kwamba ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na Afrika unategemea kufanya mikutano na mipango kadhaa inayochangia maendeleo ya bara la kiafrika.


Na Dokta Sherin Asem "Naibu wa kituo cha tafiti za Kilimo" alionyesha juhudi za kuunda mashamba ya pamoja katika nchi za kiafrika, na historia ya Misri pamoja na Afrika katika uwanja wa Kilimo, pia alielekea mtazamo na mkakati wa Wizara ya Kilimo katika nchi za kiafrika, nyanja za ushirikiano wa pamoja, na kuimarisha nchi tofauti.


Na aliwatambulisha vijana waafrika kwenye kituo cha tafiti za Kilimo, kituo cha tafiti za Jangwa na nyanja zake, na vituo vyote vinavyohusiana kwa Wizara ya Kilimo, na alizungumzia programu ya kuboresha mashamba ya kimisri katika nchi za kiafrika pamoja na miradi ya kurekebisha ardhi za Kilimo.


Na alimaliza mkutano wake kwa matembezi ya kutafutia ndani ya vituo yaliyojumuisha maabara ya tafiti, kuchunguza maji, sumu za kiasilia,uchafuzi wa kikaboni,vyanzo vya kudhibiti, teknolojia, amani ya chakula,kuchunguza na kupanga Punje, na vioevu vya kibiolojia.

Comments