Waziri wa Vijana na Michezo na Balozi wa Uhispania washuhudia uzinduzi wa kamusi ya Kiarabu-Kihispania husika katika mpira wa miguu
- 2021-02-21 15:56:04
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Balozi Ramon Khail Casarias, Balozi wa Ufalme wa Uhispania nchini Misri, walishuhudia uzinduzi wa kamusi ya kwanza ya Kiarabu-Kihispania inayohusika katika mpira wa miguu na misamiati yake.
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri huyo, alielezea furaha yake kwa kuzindua kamusi hiyo, ambayo ni hatua kubwa kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Ufalme wa Uhispania kuchangia kueneza Utamaduni kati ya nchi hizo mbili, inayoongeza upendo ya watu wawili kwa mpira wa miguu.
Akiongeza kuwa Kamusi imeshafasiriwa kutoka Kihispania kuelekea Kiarabu sanifu,iwe baadaye kubwa zaidi na ipatikane kwa wazungumzaji na wasemaji wa kiarabu, hilo ndilo ni lengo letu mwanzoni nalo ni kukuza Ushirikiano na mahusiano kati yetu.
Ameshahitimu akisema , ningependa kuchukua fursa hiyo kuelezea furaha yangu kwa Ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Ubalozi wa Uhispania katika miradi na hafla zinazofanyika kwa uratibu kati ya Wizara na ubalozi katika nyanja mbalimbali za vijana na kimichezo.
Katika hotuba yake, Balozi Ramon Khail Casarias, Balozi wa Ufalme wa Uhispania nchini Misri, alimkaribisha Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na hadhira, na akiongeza kuwa kamusi hiyo ni Ushirikiano kati ya chuo cha Cervantes na La Liga ili kukuza michezo ya Kiarabu, akiashiria kuwa kamusi hiyo ni kazi nzuri na muhtasari kwa maneno rahisi ya mpira wa miguu, na inaongeza Ushirikiano wa wanawake katika michezo na kukuza mchango wake.
Anaongeza watu wa Misri na Uhispania wanapenda sana mpira wa miguu, ambayo ni chanzo cha furaha , na kamusi hiyo inazingatiwa kama kiungo kati ya watu hawa wawili kwa mawasiliano zaidi na uhusiano wa karibu kati yao.
Khuan Fuentes, Afisa wa LaLiga huko Misri, Raquel Calia, Mkurugenzi wa masuala ya kiutamaduni wa chuo cha Cervantes, na Carole Pasteur, Mkurugenzi wa Chuo cha Cervantes, walihudhuria mkutano huo.
Comments