Waziri wa Vijana na Michezo akutana na Rais wa Shirikisho la Afrika la Mpira wa Wavu
- 2021-02-23 15:32:31
Baada ya mechi kati ya Misri na Camerun, Dokta Ashraf Sobhy alikutana na Bashri Hajij, Rais wa Shirikisho la Afrika la Mpira wa Wavu, aliyetoa shukrani zake kwa serikali ya Misri kwa kukaribisha mashindano hayo wakati wa virusi vya Corona , na kutekeleza hatua zote tahadhari na kuhifadhi Usalama na afya ya wachezaji.
Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikuwa na hamu ya kukutana na wachezaji wa timu ya kitaifa ya Mpira wa Wavu ya vijana wa Misri walio chini ya umri wa miaka 21 kwenye uwanja uliofunikwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Kairo baada ya kumalizika kwa mchezo wao uliofanyika Jumatatu jioni dhidi ya timu ya kitaifa ya Cameroon katika raundi ya pili ya Mashindano ya Vijana Afrika iliyokaribishwa kwa Misri hadi 24 Februari hii.
Timu ya kitaifa ya Vijana wa Mafarao ilishinda timu ya kitaifa ya Camerun kwa 3 -1, Timu ya kitaifa ya Misri inahitaji kushinda timu ya Morocco katika mechi ya mwisho ili kushinda taji la ubingwa baada ya ushindi wake katika raundi ya kwanza dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Waziri huyo alisisitiza usaidizi mkubwa kwa wachezaji wa timu za kitaifa katika michezo kwa aina zake zote, wakati wa mashindano yao katika michuano yote, wakati wa mfumo wa Wizara unaolenga kutoa misaada yote kwa Wachezaji kuhakikisha mafanikio kwa kuratibu pamoja na Kamati ya kiolimpiki na Mashirikisho ya kimichezo.
Comments