Betso Mosimane, kocha wa Al-Ahly, hakukasirishwa sana kwa kupoteza kwa timu yake kutoka timu ya Simba, Tanzania, katika raundi ya pili ya awamu ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Licha ya ugumu wa hisabu za mabingwa watetezi, baada ya ushindi wa Vita Club 4-1 dhidi ya Al-Merrikh nchini Sudan.
Simba iliongoza kundi kwa alama sita, ikifuatiwa na Vita Club na Al-Ahly kwa alama tatu, Wakati timu ya Sudan iko chini ya ratiba hiyo bila chochote.
Walakini, Musimane alionekana kuwa mtulivu sana katika maelezo yake baada ya mechi, akisema, "Tulipoteza mechi, lakini hatukutoka kutoka mashindano ... Lazima tushinde hali hiyo, na tumebaki na alama 12 katika michezo 4 ijayo. "
Ingawa kocha wa Afrika Kusini alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba hatatafutia sababu za upotezaji huko Tanzania, hakusahau kutaja "timu iliathiriwa kwa hali ya hewa, na ikiwa mechi ilifanyika saa kumi na moja au saa kumi na mbili, timu ingefanya vizuri zaidi, na kufanyika mechi hiyo mbele ya mashabiki ,hawezi kutoa maoni kwake, ukiwa uamuzi wa serikali. "
Lakini Pitso hakukosa nafasi hiyo kwa kusema, "Kwa kutambua kwamba mazingira hayo hayapo popote ulimwenguni wakati wa Janga la Corona."
Kocha wa Al-Ahly pia alieleza kuwa timu ilinyanyaswa na kuzuiwa kuingia uwanjani kabla ya mechi, na akaacha Jambo hilo kwa Baraza la wakurugenzi wa klabu, akisema, "Usimamizi wa kilabu utakuwa na nafasi ya kutoa maoni juu ya kile kilichotokea .. Mimi ni kocha, na jukumu langu ni kuzungumzia masuala ya kiufundi tu. "
Kocha wa Al-Ahly alikataa kutia chumvi upotezaji wa Tanzania, na alikabiliwa kwa kukosolewa kwa fikra zake za kiufundi na kimkakati kwa kutegemea wachezaji watatu kwenye safu ya kiungo, akisema, "Inawezekana kiwango cha mchezaji au timu kwa jumla inatofautiana kutoka kwa mechi moja kuelekea nyingine .. Sitaki kuonekana katika sura ya mtu asiyekubali kushindwa "
Aliongeza, "Badala yake, lazima tuweke kila kitu mahali pake , kukabiliana na hasara kwa utulivu na raha," Lazima tuunge mkono kuendelea na safari yetu ndefu, nasi tutakuwa waaminifu pamoja na nafsi zatu kuchambua sababu za upotezaji huo. "
"Betsu" hakuridhika na hilo. Badala yake, alilazimishwa kutilia mkazo methali maarufu nchini Afrika Kusini: "One Swallow doesn't make a Summer," akiongeza, "kwetu Afrika Kusini tunasema wakati ndege mmoja anaonekana akiimba angani, haimaanishi majira ya joto hufika.
Maana ya methali maarufu hiyo inaonesha kuwa mambo hayatabaki kuwa mazuri wakati wote, wakati Amr Moheb, mkalimani wa Klabu ya Al-Ahly, aliielezea katika mkutano na waandishi wa habari kwa kusema, "Kupata vizuizi mara moja, haimaanishi kuwa mambo yote ni mabaya. "
Comments