Mkakati wa sayansi, teknolojia na ubunifu 2024 wa kiafrika kwenye meza (nyumba ya sanaa ya Afrika)
- 2019-04-01 16:28:31
Wizara ya vijana na michezo iliyo chini ya uongozi wa Dk,
Ashraf Sobhi, imefanya mkutano wa pili miongoni mwa harakati za “baraza la
nyumba ya sanaa ya Afrika” ya kila mwezi kuhusu hali ya sayansi, teknolojia na
ubunifu barani Afrika. Katika wakati huo huo wa mchango wa kikanda ambao Misri
imeushughulikia kulingana na urais wake wa Umoja wa Afrika 2019.
Amehudhuria mkutano huo, Dk. Ahmed Hamdy, ambaye ni
mkurugenzi mkuu wa kamisheni ya utafiri wa kisayansi na kiufundi katika umoja
wa Afrika, Dk. Eslam Abo Almajd, ambaye ni mshauri wa waziri wa elimu ya juu na
mambo ya utafiti wa kisayansi kwa mambo ya kiafrika, Dk. Meret Rustum, ambaye
ni mwakilishi wa mabaraza ya nchi za kiarabu kwenye utafiti wa kisayansi, Bi.
Dina Fouad, naye ni mwenyekiti wa idara kuu ya bunge na elimu ya kiraia katika
wizara ya vijana na michezo, na Bw. Hassan Al-Ghazali, ambaye ni katibu mkuu wa
ofisi ya vijana wa kiafrika naye ni makamu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa
kiafrika. Mkutano huo ulikuwa ukizungumzia majadiliano ya nafasi na changamoto
maalumu katika nyanja za kisayansi na kiteknolojia ndani ya bara la Afrika, na
jinsi zinavyoathiri vijana wa bara la Afrika.
Dk. Ahmed Hamdy, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kamisheni ya
utafiri wa kisayansi na kiufundi katika umoja wa Afrika, amesisitiza umuhimu wa
utafiri wa kisayansi hasa ndani ya bara la Afrika na umuhimu wa kuunganisha
maudhui za utafiti wa kisayansi na vijana kwenye uwanja wa uongozi wa kazi
(shughuli), akiashiria mchango wa utafiti wa kisayansi katika ushirikiano wa
utatuzi(ufumbuzi) wa matatizo ya bara la Afrika katika nyanja tofauti tofauti.
Na Bw. Hamdy akiongezea kwamba utilianaji umuhimu wa
kisayansi na kiteknolojia katika sehemu zenye mizozo au migogoro ya kibinadamu
utasaidia katika kutatua au kusuluhisha masuala, matatizo na changamoto
zilizolikabili bara la Afrika. Akithibitisha kwamba maono na mkakati wa Misri
kwenye malengo ya mwaka 2030 unawezekana kutekelezwa kwa kupitia msaada wa
vijana hodari na kupitia teknolojia, sayansi na ubunifu.
Na kwa upande wake, Dk. Eslam Abo Al-Majd, ambaye ni mshauri
wa waziri wa elimu ya juu na utafiri wa kisayansi kwa mambo ya bara la
kiafrika, ameashiria kwamba: wizara ya elimu ya juu na utafiri wa kisayansi
inaahughulikia daima kwa utilianaji umuhimu wa kuwafundisha vijana umuhimu wa
bara lao la Afrika na kuwajulisha bara hilo hasa kwamba wao ndio wanaowakilisha
nguvu tegemezi zinazoendesha nyanja zote, licha ya kuwepo changamoto kubwa
zinazolikabili bara hilo.
Akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa vyuo vikuu kwenye
kiwango cha kikanda katika nyanja za utafiti wa kisayansi na kutoa vipaumbile
katika utekelezaji wa mikakati hiyo.
Na Dk. Meret Rustum, ambaye ni mwakilishi wa umoja wa
mabaraza ya nchi za kiarabu kwenye utafiti na sayansi, ameeleza misingi ya
kuchagua maudhui ya misaada iliyotolewa kwa vijana ambayo inabudi kuafikiana
nkukubaliana na mipango ya kimikakati ya nchi, na ambayo inachangia kwa kiwango
kikubwa katika kukamilisha mipango ya nchi katika nyanja zenye vipaumbile.
Aidha inachangia utanuzi (upatikanaji) wa nafasi za
ushirikiano katika taasisi mbalimbali za mambo ya utafiti wa kisayansi.
Akiashiria kwamba lengo kuu la michango ya misaada hiyo ndiyo kuwafundisha vijana
watafiti wanaoshiriki kwa namna ya kuongoza utafiri wa kisayansi katika nyanja
za sayansi na teknolojia na kuboresha ujuzi wao wa kielimu na kutekeleza baadhi
ya malengo ya kimaendeleo na kutumia vizuri rasilimali na nafasi za kiutafiri
zinazopatikana kupitia ushirikiano wa pamoja.
Vijana wa Afrika wanaoshiriki katika baraza wamejadiliana
changamoto za utafiri wa kisayansi na matatizo yanayowakabili vijana katika
nyanja ya kiteknolojia na sayansi za kiubunifu na miongoni mwa matatizo hayo ni
tatizo la ufadhili wa fedha, na ugumu wa kunufaika kwa vijana kutokana na
misaada, na hali ya watafiti ya kifedha. Kama pia, baadhi ya vijana watafiri
wameonesha majaribio yao ya kisayansi na ya kiutafiti na vumbuzi na undaji zao
ili kujadiliwa pamoja na wahusika.
Comments