Timu ya kitaifa ya Misri yashinda medali ya fedha ya mashindano ya Baiskeli ya Afrika kwa wasichana


Mashindano Siku ya pili  ya Baiskeli ya Afrika Namba 15 ya Barabara yanayofanyika mnamo kipindi cha Machi 2 hadi 6 Machi huko mji wa 6 Oktoba,yalishuhudia mashindano makali na mazito.


Misri ilishinda nafasi ya pili katika mashindano ya barabara Mmoja kwa Wachipukizi "Dhidi ya saa", ambapo mchezaji wa Misri Habiba Elewa alishinda nafasi ya pili, na akashinda fedha katika mashindano kwa wasichana baada ya kumaliza mbio za km 13.5 kwa muda wa dakika 25, sekunde 24 na Sehemu 11 ya sekunde.


Mchezaji wa Afrika Kusini Shanti Oliver alikuja katika nafasi ya kwanza, sekunde 3 tu kabla ya bingwa wa Misri, wakati Nasreen Hawili mchezaji wa Algeria alishika nafasi ya tatu.


Katika mashindano ya wachipukizi, mchezaji wa Afrika Kusini Pedri Cruz alishika nafasi ya kwanza, Etienne Twisieri alishika wa pili, na mchezaji wa Afrika Kusini Justin Chestron alishika nafasi ya tatu.


Katika mashindano ya jumla ya wanaume, wachezaji wawili wa Afrika Kusini, Ryan Gibbons na Kent Main, walikuja katika nafasi ya kwanza na nafasi ya pili, wakati wa Rwanda Moise Mugisha alikuja katika nafasi ya tatu.


Katika mashindano ya wanaume chini ya miaka 23, mchezaji wa Algeria Hamza Mansouri alishika nafasi ya kwanza, wachezaji wa Rwanda Jean-Eric Habimana alishika nafasi ya pili, na Mburkini Paul Demont alishika nafasi ya tatu.


Katika mashindano ya jumla ya wanawake, wachezaji  wa Afrika Kusini  Carla Uroberhorzr, Janci Van Rassenberg walishika nafasi ya kwanza na ya pili mfululizo, na mchezaji wa Namibia Vera Adrian alishika nafasi ya tatu.


Na katika mashindano ya wasichana chini ya miaka 23, Mchezaji wa Afrika Kidini Van Rasnberg alishika nafasi ya kwanza,na Wachezaji wawili wa Rwanda

  Jacqueline Tuichemi na Diane Ingabire, walikuja katika nafasi ya  pili na tatu mfululizo.


Kulingana na utaratibu wa mwisho wa wachezaji kwenye mashindano , wachezaji wanapata alama zinazoongezwa kwa uainishaji wa ulimwengu kulingana na nafasi zilizopatikana.

Comments