Waziri wa Michezo ahudhuria sherehe ya Kamati ya Parlimpiki kuwaheshimu mabingwa 50 wa Misri


Leo, Jumapili , Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia kuheshimiwa kwa mabingwa 50 wa Walemavu katika hafla iliyoandaliwa na Kamati ya Walemavu ya Misri kwa kushirikiana na Kampuni ya Allianz huko Misri.


Sherehe imejumisha semina mbili za kielimu, ya kwanza kuhusu maandalizi ya kisaikolojia, na ya pili kuhusu ya lishe bora, ili kutoa huduma bora na msaada kwa mabingwa wa Paralimpiki.


Hafla hiyo ilihudhuriwa na Dokta Hayat Khattab, Mwenyekiti wa Kamati ya Walemavu ya Misri, Ibrahim Amin, Mjumbe wa Bodi, Meja Jenerali Mohamed Nour, Dokta Amr Haddad, Waziri Msaidizi wa Vijana na Michezo, Ayman Hegazy, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kikundi cha Makampuni Allianz nchini Misri, na Mina Abd El Shahid, Mkurugenzi Mtendaji wa Sekta za Usimamizi wa Soko la Kikundi  cha Allianz, Misri.


Katika hotuba yake, Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kutoa msaada kamili na utunzaji kwa mabingwa wa Olimpiki na Paralympiki wa Misri katika michezo mbalimbali, wakifanya kazi kutimiza madai yao, na kufuata mipango ya mafunzo waliyopewa kwa kujiandaa na mashindano ambayo wanashiriki katika uratibu pamoja na Kamati ya Olimpiki, Kamati ya Walemavu na Mashirikisho ya Michezo.


Waziri huyo alielezea uwezo wa mashujaa wa Ulemavu wa Misri kwa changamoto na kufanikiwa katika mashindano wanayoyapambana, na kufikia mafanikio ya kipekee na idadi ya rekodi za ulimwengu zinazoonesha umahiri wao na nguvu ya dhamira yao ili kuinua hadhi ya nchi yao katika vikao anuwai vya kimataifa.


Kwa upande wake, Dokta Hayat Khattab alisema, "Tuko mwanzoni mwa Olimpiki ya Tokyo ya 2021, na pamoja na pande zote zinazohusika na kuwapa nguvu mabingwa wa Paralympiki huko Misri, Kamati ya Walemavu ya Misri itaweza, kupitia msaada na ufadhili wa Wizara ya Vijana na Michezo na kwa kushirikiana na Allianz huko Misri, kuandaa mpango kamili wa ukarabati  unaojumuisha msaada wa maadili na nyenzo. "Kwa mashujaa wa wanariadha wa Misri, na kuongeza utendaji wao wa kitaalam kushinda nafasi za juu zaidi katika michezo anuwai katika mashindano makubwa ya kimataifa na Duniani. 


Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni ya Allianz huko Misri alisema: "Allianz daima inathamini Misri na juhudi kubwa zinazofanywa kwa Wizara ya Vijana na Michezo na Kamati za Olimpiki na Paralympiki pia kuendeleza viwango vya michezo nchini Misri, na tuko Allianz katika Misri, na kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, tumeshirikiana na Kamati ya Walemavu ya Misri katika mipango mingi ya kusaidia wanariadha wa Misri, na sasa tunajivunia tuwe mshirika wa bima ya ulimwengu kwa harakati za kimataifa za Olimpiki na Paralympiki kuanzia 2021 hadi 2028, itakayokuwa na athari kubwa kwa msaada wetu kwa wanariadha wa kitaalam wa Misri. "


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Sekta za Usimamizi wa Soko la Kikundi cha Allianz huko Misri alielezea kuwa tabia chanya ya wanariadha wetu na maadili ya kijamii ambayo Allianz huko Misri wanashirikiana na Wizara ya Vijana na Michezo na Kamati ya Walemavu ya Misri inastahili uangalifu mkubwa zaidi, akiongeza kuwa tutafanya kazi kwa bidii kutumia utaalam wetu katika uwanja wa bima na kuongeza faida kutoka kwa ushirikiano wetu. Pamoja na taasisi za kimataifa na za mitaa kurekebisha na kusaidia mashujaa wetu kisaikolojia, kimwili na kiakili. "

Comments