Baraza la Kitaifa la Wanawake lamshukuru Rais El_Sisi kwa kutoa maagizo ya kuwepo kwa wanawake katika Baraza la Nchi
- 2021-03-13 21:33:05
Baraza la Kitaifa la Wanawake linaloongozwa na Dokta Maya Morsi, washiriki wake wote wa kike na wajumbe wa baraza hilo wanatoa shukrani na Heshima kubwa sana kwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa kutoa maagizo leo kwa Kansela Omar Marawan, Waziri wa Sheria, kwa kushirikiana na Rais wa Baraza Kuu la Mahakama na Rais wa Baraza la Nchi, kuwepo kwa wanawake katika majukumu hayo mawili ili kuamsha haki ya kikatiba kwa usawa na kutobaguliwa, wakati wa Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.
Na Dokta Maya Morsi alielezea furaha yake kubwa na kiburi kwa uamuzi huo, akisema : "Hiyo ni habari nzuri zaidi katika Siku ya Wanawake Duniani." Aliendelea: "Maagizo ya Rais leo yanazingatiwa kuvunja kizuizi kinachopatikana mbele ya wanawake wa Misri katika Baraza Kuu la Majaji na Baraza la Nchi, na Haki mpya imeoongezwa kwa faida nyingi za mwanamke huyo wa Misri, zilizofanikiwa kwake wakati wa enzi yake ya dhahabu, wakati wa kuwepo kwa utashi wa kisiasa ambao siku zote unahakikisha haki kwa mwanamke wa Misri. "
Comments