Asubuhi ya leo, Jumanne, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, ameshafika, na ujumbe wake ulioandamana naye wakielekea Diwani kuu ya Mkoa wa Fayoum, kufungua na kukagua miradi kadhaa ya vijana na michezo ndani ya mkoa huo, na kuupongeza kusherehekea siku yake ya kitaifa.
Waziri huyo amepokelewa na Dokta Ahmed Al-Ansari, Gavana wa Fayoum, Meja Jenerali Abdel-Rahman Shalash, Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Kurugenzi la Michezo huko Fayoum, na wakuu watendaji wa Mkoa.
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliwapongeza Mkoa wa Fayoum na wakuu wake katika hafla ya Siku ya Kitaifa ya Mkoa huo, ambayo ni sawa na Machi 15, kuadhimisha msimamo wa watu wa Fayoum dhidi ya uvamizi wa Uingereza wakati wa mapinduzi ya 1919.
Inaamuliwa kuwa Ziara ya Waziri wa Vijana na Michezo kwa Fayoum itajumuisha ufunguzi wa miradi kadhaa ya vijana na michezo ndani ya mkoa huo, pamoja na vituo vya vijana vya Tabhar, Adwa, Mizar, na klabu za Al Safwa , Qarun, pia Waziri huyo atafanya mkutano wa mazungumzo wazi pamoja na vijana wa Mkoa wa Fayoum.
Ziara ya Waziri huyo huko Mkoa wa Fayoum inakuja katika mfumo wa ziara zake za ukaguzi wa vituo vya vijana na michezo katika Mikoa tofauti ya Jamhuri, kufuatilia maendeleo ya kazi na kujua maendeleo yake ya hivi karibuni.
Comments