Waziri wa Vijana na mwenzake wa Sudan Kusini wakutana na vijana katika mazungumzo wazi
- 2021-04-02 09:28:07
Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri Dk. Ashraf Sobhy na mwenzake wa Sudan kusini Dk Albino Paul wanakutana na vijana wa Sudan Kusini katika mazungumzo wazi wakati wa shughuli za Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini, unaoandaliwa kwa (Idara kuu kwa Programu za Kiutamaduni na Hiari - Ofisi ya Vijana wa Afrika) kwa kushirikiana na Umoja wa Kitaifa wa Vijana wa Sudan Kusini na Wizara ya Vijana na Michezo ya Sudan Kusini na Chuo Kikuu cha Kairo, Tawi la Khartoum, kama sehemu ya mradi wa "Umoja wa Bonde la Nile ... Maoni ya Baadaye" katika toleo lake la tatu chini ya kauli mbiu ya "Kwa ajili ya Sudan Kusini", utakaofanyika katika kipindi cha kuanzia Aprili 3 hadi 8, 2021 katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi.
Katika shughuli za Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Kairo kwa vijana wa Sudan Kusini, viongozi 200 wa vijana kutoka kikundi cha umri wa miaka 18 hadi 35 kutoka jinsia zote watashiriki, pamoja na watu wenye ushawishi mkubwa zaidi katika jamii, kama wanaharakati wa Jamii ya kiraia na wasomi katika nyanja tofauti tofauti, pamoja na waandishi wa habari na wataalam wa vyombo vya habari pamoja na vijana wamisri watafiti katika faili la nchi ya Sudan Kusini.
Ajenda ya mkutano huo ni pamoja na kushughulikia dhana ya nchi ya kitaifa ikiwakilishwa kwa kushughulikia mahusiano ya pande mbili kati ya Sudan Kusini na Misri na juhudi za serikali ya kitaifa katika maendeleo, mchango wa sekta binafsi katika kujenga vyombo vya habari vya kitaifa, njia za kukabiliana na uvumi wa Vyombo vya habari na maoni yasiyo kweli, kujadili mchango wa Mwanamke katika hati za bara, na kuonesha uzoefu wa uratibu kwa vyama vya vijana, pia kugusa mchango wa Wizara ya Vijana ya Misri na Umoja, pia kuonesha uzoefu wa mpango wa "Bonde la Nile, Uchumi wenye ubunifu, na kushughulikia jukumu la Kameshina ya Umoja wa Afrika na athari za kuharibu kwa mfumo wa Ada na Maadili juu ya Usalama wa kitaifa na njia za kukabiliana na Ufisadi na kuonesha mifano bora zaidi, pamoja na kujadili mchango wa taasisi za udhibiti kwa Ufuatiliaji na Tathmini, pamoja na kufanyika Warsha kadhaa kuhusu Utamaduni wa mazungumzo, Malezi ya kiraia, na mchango wa vijana katika kujenga nchi ya kitaifa
Comments