Waziri wa Michezo ampongeza Samar Hamza baada ya kufikia Olimpiki ya Tokyo


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alimpongeza nyota wa timu ya kitaifa ya Mieleka ya wanawake, Samar Hamza Uzani wa, 76 k baada ya ushindi wake dhidi ya bingwa wa Tunisia na kupata kwake kadi ya kufikia Olimpiki katika mechi za fainali za Afrika huko Tunisia katika kipindi cha Aprili Mosi hadi  Aprili 4, 2021.


Ikumbukwe kwamba timu ya kitaifa ya Mieleka ya wanawake inashirikiwa na wachezaji 4 kwenye mechi za fainali za Afrika kufikia Olimpiki, nao ni (Nada Madani, Uzani wa 50 K - Iman Essam, Uzani wa 57 K - Enas Khurshid, Uzani wa 68 K - Samar Hamza, Uzani wa 76 K)


Kupitia simu pamoja na Rais wa Shirikisho la Mieleka la Misri, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza hitaji la wanariadha wa kike kufanya kila juhudi kupata kadi za kufikia Olimpiki kwa mechi zijazo, wakitakia mafanikio kwa ujumbe wa kimisri wanaoshiriki katika mashindano na kupata idadi kubwa zaidi ya kadi za kufikia Olimpiki kwa wachezaji wengine kutoka kwa Mieleka ya wanawake na ya huru.


Ikumbukwe kwamba Wizara ya Vijana na Michezo imetoa msaada wa kifedha kwa Shirikisho la Mieleka la Misri tangu mwanzo wa programu ya maandalizi na kufikia Olimpiki hadi sasa, karibu paundi milioni 12.5, pamoja na mpango wa udhamini wa kibinafsi uliotolewa kwa Wizara ya Vijana na Michezo na sekta binafsi kwa wachezaji 3 kutoka timu za kitaifa kwa ajili ya Mieleka, na hii inakuja katika mfumo wa juhudi zinazoendelea za Wizara kusaidia mfumo wa Mieleka wa Misri kuwafikia kwa matokeo bora katika hafla zote za kimataifa.


Ikumbukwe kwamba Wizara ya Vijana na Michezo inazingatia sana timu anuwai za Mieleka, sawa kwa  upande wa kifedha au kinafsi , kwa sababu ya uwakilishi mzuri katika Olimpiki zijazo huko Tokyo, na kushindana zaidi ya medali moja ya Olimpiki.

Comments