Waziri wa Vijana na Michezo azindua shughuli za Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini


Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Dokta Albino Paul, Waziri wa Vijana na Michezo wa Sudan Kusini, walizindua shughuli za Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini, ulioandaliwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo kupitia (idara ya Vyuo Vikuu - Ofisi ya Vijana wa kiafrika) kwa kushirikiana na Umoja wa Kitaifa wa Vijana wa Sudan Kusini na Vijana wa Wizara na Michezo ya Sudan Kusini na Chuo Kikuu cha Kairo, Tawi la Khartoum, kama sehemu ya mradi wa "Umoja wa Bonde la Nile ... toleo lake la tatu chini ya kauli mbiu ya "Kwa ajili Sudan Kusini ", inayofanyika katika kipindi cha 3 hadi Aprili 8, 2021, Aprili 3 hadi 8, 2021 katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi.


Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa mahusiano kati ya Misri na Sudan Kusini ni thabiti yaliyoanza tangu karne kadhaa, kwani Mto Nile, ambao ni damu ya nchi hizo mbili, unaziunganisha, na unganisho kati ya nchi hizo mbili ulionekana katika hali tofauti. , akimaanisha Sudan ambayo ina umuhimu wa kipekee kwa Misri, kwa sababu ya kina ya Usalama na kimkakati, pamoja na mahusiano makubwa ya kihistoria, kwani ndio msingi wa mkutano na mawasiliano ya Waarabu na Waafrika.


Sobhy aliongeza, "Kuna nafasi na makubaliano tofauti kati ya nchi hizo mbili, ndani ya mfumo wa dhamira ya kuheshimiana kuimarisha mifumo ya ushirikiano kati yao, na pia kushughulikia maendeleo muhimu zaidi ya kisiasa yanayohusiana na masuala ya kikanda na bara yenye masilahi ya pamoja," akisisitiza msaada wake kamili kwa bara la Afrika, haswa Sudan Kusini.


Dokta Albino Paul alielezea furaha yake kubwa kushiriki katika mkutano huo,  unaopanua madaraja ya mawasiliano kati ya nchi hizo mbili na kuongeza mahusiano ya pande mbili kati ya ndugu wawili, pamoja na kuwa fursa kwa vijana kubadilishana maoni na uzoefu wao wakati wa mkutano, akimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa kuandaa mkutano huo na kujitahidi kuongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kiwango cha vijana.


Waziri wa Vijana na Michezo wa Sudan Kusini, aligusia hafla ya kihistoria iliyoandaliwa kwa Jamuhuri ya Kiarabu ya Misri, Sherehe ya kuhamisha Masanamu, iliyoathiri kikubwa  ulimwenguni kote, akisisitiza utukufu na uhalisi wa historia ya Misri kwa zama zote, akishukuru uongozi wa kisiasa kwa msaada endelevu wa Sudan Kusini.


Shughuli za Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini zinafanyikwa na viongozi 200 wa vijana kutoka umri wa miaka 18 hadi 35  kutoka kwa jinsia zote mbili, pamoja na vikundi vyenye ushawishi mkubwa katika jamii, wanaowakilishwa na wanaharakati wa jamii na wasomi katika nyanja zao anuwai, mbali na waandishi wa habari na wataalam wa vyombo vya habari, pamoja na vijana wa Misri Watafiti katika faili ya Sudan Kusini.

Comments