Waziri wa Michezo ashiriki katika mikutano ya Ofisi ya Afrika ya Wakala wa Kimataifa wa Kupambana dawa za kusisimua misuli
- 2021-04-15 19:28:18
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Kimataifa wa Kupambana dawa za kusisimua misuli (Wada), alishiriki pamoja na Bi Amira Al-Fadhel, Mratibu wa Umoja wa Afrika kwa Afya, Ustawi wa binadamu na Maendeleo ya Jamii, Bwana Rodney Swegler, Mkurugenzi wa Ofisi ya kiutendaji ya Kupambana dawa za kusisimua misuli kwenye Bara la Afrika (Rado), na Bwana Masha, Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Afrika, na wawakilishi wa Ghana na Afrika Kusini, kujadili njia za ushirikiano mnamo siku zijazo.
Mkutano ulijadili masuala kadhaa ya pamoja , haswa yale yanayohusiana na msimamo wa Misri kama mwanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Kupambana na Dawa za kusisimua misuli kwa upande wa michango yake na kwa kufuata sheria kama nchi za Kiafrika, na kusaidia wanariadha kupitia kusikia sauti yao na kuonesha jukumu la michezo safi, pia Hadhara walikubaliana kuunganisha sauti ya Kiafrika katika mkutano ujao mnamo mwezi wa Mei.
Waziri huyo alisisitiza kuwa mkutano huo unakuja katika mfumo wa ushirikiano wa kimataifa katika uwanja wa kupambana na utumiaji wa dawa za kusisimua misuli katika michezo na jukumu muhimu ambalo Misri inacheza kimataifa,
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisema kuwa : Misri ina matarajio makubwa kwa michezo kutokuwa na dawa za kusisimua misuli barani Afrika na ulimwenguni, akiashiria kuwa Misri itatoa msaada wa kila aina kwa Wakala wa Kimataifa wa Kupambana dawa za kusisimua misuli kufikia malengo yake. malengo katika suala hilo.
Sobhy pia alisisitiza jukumu Chanya la Shirika, ofisi ya kiutendaji na tume kwa uungwaji mkono wao kamili kwa kutoa idhini kwa Maabara ya Kimataifa ya Uchambuzi wa Matibabu kwa dawa za kusisimua misuli.
Comments