Waziri wa Michezo: Misri yajiandaa kuanzisha kituo kikubwa zaidi cha michezo huko Tanzania


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia mkutano wa vyombo vya habari ili kutangaza uzinduzi wa Wizara kwa moja ya miradi yake mikubwa ya michezo barani Afrika; kuanzisha vituo vya michezo na vijana vya Misri kuanzia nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Kampuni ya( I FRENDS SPORT), Katika mfumo wa kuimarisha mahusiano kati ya Misri na nchi za bara la Afrika katika uwanja wa michezo, na hayo yote kwa mahudhurio ya Balozi Ahmed Mustafa, Naibu wa Waziri  Msaidizi wa Mambo ya Nje kwa Nchi za Bonde la  Mto Nile,  Bw.Amr Mostafa Kamel, Mkuu wa Kampuni ya kiutendaji, na viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo .


Waziri wa Vijana na Michezo ameshasema: "Misri inajiandaa kuanzisha kituo kikubwa zaidi cha michezo nchini Tanzania kama kiini cha vituo vingine barani Afrika, kwa kuzingatia mahusiano ya Misri na Afrika yanayotofautisha kwa Upweke na kuheshimiana pamoja tangu kuanzishwa kwake, haswa kwa kuzingatia mahusiano thabiti ya kindugu katika ngazi ya Kiafrika kati ya serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na nchi za Kiafrika, na kile kinachosababisha Uchanya  kwa mahusiano yote ya Mielekeo yake rasmi, katika ngazi ya kisiasa, kiuchumi, na katika  Mwelekeo wake wa kienyeji kiutamaduni, kijamii, na kibiashara, na Ufuatiliaji wa michezo haswa, kama moja ya njia muhimu zaidi ya hatua ya pamoja.


Akiongeza, "Dharura ya kufanya kazi kwa kuanzisha mizizi ya urafiki na Ndugu iliopo kati ya serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na serikali za nchi za Kiafrika, na kukuza mahusiano na Ushirikiano wa kimichezo ndani ya mfumo unaotawaliwa kwa malengo kadhaa ya pamoja, la muhimu zaidi  ni kufanya kazi pamoja kusaidia shughuli za michezo na vijana katika nchi za Kiafrika, ambalo lina athari yake nzuri juu ya malezi ya watu wa Kiafrika. "


Sobhy alisisitiza kuwa ushirikiano huo uko katika mfumo wa shime ya Uongozi wa kisiasa barani Afrika kufungua maeneo mengi ya kuhudumia nchi na mawasiliano endelevu kukuza mahusiano katika nyanja tofauti na kuhamasisha sekta binafsi na wafanyabiashara wa Misri kugundua masoko ya nchi hizo na kupata nafasi za uwekezaji kwa njia ambayo hutumikia masilahi ya pamoja kati ya nchi na kuimarisha mahusiano katika nyanja anuwai, ambapo wa muhimu zaidi ni  uwanja wa michezo, akiashiria kwamba mradi huo unapangwa kutekelezwa katika nchi kadhaa za Kiafrika kwa kushirikiana pamoja  na Wizara ya Misri ya Mambo ya nje.


Waziri wa Michezo ameongeza kuwa uzinduzi wa Wizara kwa mradi mkubwa wa michezo wa kuanzisha vituo vya michezo na vijana kuanzia nchini Tanzania, umeangaliwa na kuwasilishwa kwa Baraza la Mawaziri kuutathmini, na kuuangalia, kisha kuuidhinisha, na kwa hivyo tuliweza kukuza upeo na kuvutia uwekezaji wa michezo.


Kwa upande wake, Balozi Ahmed Mustafa alisifu juhudi za Wizara ya Vijana na Michezo zinazolenga kutia undani zaidi katika nchi za Afrika na kuanzisha vituo anuwai vya vijana na michezo, itakayokuza utamaduni wa kuungana na mawasiliano kati ya Misri na watu wa Afrika, haswa vijana ya bara la Afrika, akisisitiza kuwa mwanzo huo huko Tanzania utakuwa kiini cha mwanzo mpana katika uwanja wa michezo, vijana wa Misri na Waafrika.


Wakati wa hotuba yake, Amr Mostafa Kamel, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ( I Friends Sport), alisema kuwa kampuni hiyo, kwa kushirikiana na Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri, iliangalia kuanzishwa kwa vituo vya michezo na vyuo vya mpira wa miguu katika bara la Afrika baada ya kutembelea nchi nyingi za Kiafrika, akiashiria kuwa awamu ya kwanza ya mradi inaanzia  huko mashariki mwa Bara, akisisitiza kuwa kusudi la kuanzisha vituo ni kuimarisha kuwepo kwa kimisri barani Afrika kama nguvu laini, ikizingatiwa Tanzania ni moja ya nchi muhimu zaidi za Kiafrika, na kuwekeza katika uwanja wa michezo kwa kufanya vyuo vya michezo na mapato ya kifedha, na vile vile kuuza bidhaa kwa mmea wa nyasi bandia kwa kushirikiana na Wizara ya Vijana na Michezo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (I Friends Sport)  aligusia vifaa vya kituo cha michezo cha Misri kinachopangwa kuanzisha, ambacho ni pamoja na Viwanja vya "Mpira wa miguu, mafunzo na  kisheria, uwanja anuwai kwa mpira wa Kikapu, mpira wa wavu na mpira wa mikono,  bwawa la kuogelea la olimpiki, uwanja wa tenisi, kituo cha mazoezi ya usawa wa mwili kwa michezo yote, Eneo maalum kwa Michezo ya Nguvu, Kituo cha Tiba ya Michezo na Tiba ya Kimwili kwa Wanariadha na Majeruhi Wasio wa Wanariadha, Taasisi ya Mafunzo, Mafunzo na Ukarabati wa Wakufunzi wa Kitaifa wa Wakuu wa Michezo, Maonesho ya Kuuza Bidhaa za kimisri Bidhaa, Kliniki za Tiba, Jengo la Utawala, Maeneo ya Kijani, Vikao vya Wanachama na korido za Inter-Look.


Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, itifaki ya ushirikiano ilisainiwa kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na kampuni ya "I Friends Sport." Itifaki hiyo ilisainiwa na Mwakilishi wa Wizara ya Vijana na Michezo, Dokta Ahmed Al-Sheikh, Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara, na Amr Mostafa Kamel, anayewakilisha kampuni inayotekeleza mradi huo.


 Kutoka Wizara ya Vijana na Michezo, Dokta Sonia Dunia, Mkuu wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Michezo, Hoda Ayoub, Mkuu wa Idara kuu ya Uwekezaji wa Michezo - Muhammad Al-Khashab, Mwenyekiti wa Kampuni ya Modon, Dokta Amr Al-Haddad, Waziri Msaidizi wa Vijana na Michezo - na Dokta Ahmed Jumaa, Waziri Msaidizi wa Vijana na Michezo  wamehudhuria mkutano huo, pia  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Ahmed Mustafa - na wawakilishi kadhaa wa mashirika na kampuni zinazoshiriki, pamoja na Ahmed Abbas, mshauri wa kiufundi wa kampuni inayotekeleza, Fadi Qaldas, na wengine wamehudhuria mkutano huo.

Comments