Timu ya kitaifa ya wasichana ya Kata yashinda Shaba katika Ligi ya Karate ya Dunia huko Ureno

Timu ya Kitaifa ya wasichana ya Kata ilishinda medali ya Shaba katika Ligi ya Karate ya Dunia inayokaribishwa huko mji wa Ureno wa Lisbon  katika kipindi cha Aprili 30 hadi Mei 3 kwa Ushiriki wa nchi 85, ambapo michuano hiyo pamoja na Mashindano ya Ulaya ni Michuano ya mashindano ya mwisho ya kimataifa ambayo inaruhusu wachezaji kufikia Olimpiki kupitia Uainishaji.


Timu ya kitaifa ya Misri ilishinda medali ya Shaba baada ya kuishinda timu ya kitaifa ya Uhispania.


Hiyo ilikuja baada ya timu ya kitaifa ya wasichana ya Kata kupata kwa jumla katika mechi za fainali 23.66, kushindana na timu ya Uhispania kwa medali ya Shaba.


Misri inashiriki katika Ligi ya Dunia kwa ujumbe mkubwa wa wachezaji 22.

Timu hiyo inaongozwa na  Hani Qeshta, kocha wa timu  ya kumite ya kike, Dokta Muhammad Abdul Rahman Muhammad Ali, Kocha wa kumite ya kiume, na Muhammad Abd al-Rijal, Hassan Gouda Hassan, kocha wa kumite, Ibrahim Magdi Musa, kocha wa Kata, na Dokta Imad Al-Sirsi, Refa wa kimataifa, Haitham Farouk, Refa wa kimataifa anayeandamana naye,  Dokta  ya timu Mahmoud Al-Rifai, na Dokta Ahmed Al-Sawy, mtaalam wa Tiba ya kimwili, wakati mambo ya timu ya usimamizi hushikiliwa na  Ahmed Abdel-Aal kama msimamizi

Comments