Yasmine Hamdy ashinda fedha kwenye ligi ya Dunia ya Karate huko Ureno


Yasmine Hamdy, mchezaji wa timu ya kitaifa ya Karate, alishinda medali ya fedha kwa mashindano ya uzito wa chini ya kilo 55, katika Ligi ya Karate ya Dunia inayokaribishwa huko mji wa Ureno wa Lisbon  katika kipindi cha Aprili 30 hadi Mei 3 kwa Ushiriki wa nchi 85, ambapo michuano hiyo pamoja na Mashindano ya Ulaya ni Michuano ya mashindano ya mwisho ya kimataifa ambayo inaruhusu wachezaji kufikia Olimpiki kupitia Uainishaji.


Yasmine alishinda fedha baada ya kupoteza mechi ya fainali  kutoka Anzelika Terlioga mchezaji wa wa ukreni katika fainali, kwa  6-0.


Yasmine Hamdy alifikia mechi ya fainali , baada ya kumshinda Tuba Yakan mchezaji wa Uturuki,kwa  8-0.


Yasmine alihakikisha  safari nzuri kwenye michuano, akifungua mechi zake kwa kumshinda mchezaji wa Slovakia Hana Kuklova kwa 5-0, kisha kumshinda Veronica Brunori wa Italia kwa 10-2, ili akutane na Yvette Goranova kutoka Belarus na kumshinda kwa 3-0.


Misri inashiriki katika Ligi ya Dunia kwa ujumbe mkubwa wa wachezaji 22. Timu hiyo inaongozwa na  Hani Qeshta, Kocha wa timu  ya kumite ya kike, Dokta Muhammad Abdul Rahman Muhammad Ali, Kocha wa kumite ya kiume, na Muhammad Abd al-Rijal, Hassan Gouda Hassan, kocha wa kumite, Ibrahim Magdi Musa, Kocha wa Kata, na Dokta Imad Al-Sirsi, Refa wa kimataifa, Haitham Farouk, Refa wa kimataifa anayeandamana naye,  Dokta  ya timu Mahmoud Al-Rifai, na Dokta Ahmed Al-Sawy, mtaalam wa Tiba ya kimwili, wakati mambo ya usimamizi ya timu hushikiliwa na Ahmed Abdel-Aal kama msimamizi.

Comments