Idara ya Maendeleo ya Michezo kwenye Wizara ya Vijana na Michezo ni mshiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili chini ya Usimamizi wa Rais wa Jamhuri
- 2021-05-14 20:04:21
Idara ya Maendeleo ya Michezo, ambayo ina idara nne za umma, nazo ni Utawala Mkuu wa Msingi wa Watu, Utawala Mkuu wa Harakati za Wanafunzi, Utawala Mkuu wa Elimu ya Jumla na Azhar,
na Utawala Mkuu wa Mashirikisho tofauti inazingatiwa kama sekta husika kwa kupanua msingi wa mazoezi ya michezo kati ya vijana kama miradi ya kitaifa kwa vijana, wanawake na walemavu, kuhamasisha raia wote kufanya mazoezi ya michezo ili kutoa nafasi kwa wengi wao kufanya mazoezi na kushiriki, kuangalia awamu zote za umri katika michezo na kupambana na magonjwa ya kisasa kupitia mazoezi ya michezo na kuwaelimisha kwa athari zake katika nyanja zote za maisha, na vile vile kurekebisha upotovu wa kitaifa, kukuza maarifa za kimsingi kwa walemavu, na kuwajihusisha pamoja na jamii kupitia mazoezi ya michezo.
Miongoni mwa shughuli hizo, kwa mfano tu ni mikutano ya pwani ya wasichana na vijana, inayotekelezwa katika vituo vya mafunzo kwa mpira wa wavu wa Pwani karibu na mikoa kumi kueneza taarifa ya mpira wa wavu wa pwani kati ya vizazi wajao, na kutoa nafasi kwa kufanya mazoezi ya shughuli pendwa za michezo katika nyanja tofauti, na pia kuongeza ufanisi wa kimwili na kuwekeza wakati wa ziada.
Na pia Mradi wa Kitaifa wa Baiskeli na Vituo vya Mafunzo, zimetekelezwa katika vituo vya mafunzo kwa Baiskeli katika mikoa yote ya Jamhuri, inayokusudia kutumia Baiskeli hiyo kama chombo cha kimsingi badala ya njia nyingine za mawasiliano zinazotumia mafuta kupunguza uchafuzi wa mazingira, kuongeza ufanisi wa kimwili na kuwekeza wakati wa ziada.
Comments