Wizara ya Vijana na Michezo yatangaza takwimu za waombaji kushiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la pili, chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri

Wizara ya Vijana na Michezo imetangaza takwimu za waombaji kushiriki katika kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa chini ya kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini", uliopangwa kuanza Juni Mosi hadi Juni 15, 2021 huko Kairo.
Wakati ambapo watu 1317 wamesajili, kiasi cha wanawake kilikuwa karibu na 41.7%, wakati kiasi cha wanaume kilikuwa karibu na 58.3%, na wastani wa umri wao ulikuwa kati ya miaka kuanzia 25 hadi 35 kama 55.8% ya jumla yao, wakati kiasi cha wale ambao umri wao ulikuwa kati ya 20 hadi 25 kilikuwa Karibu na 32.6%, wakati kiasi cha wale wenye umri wa miaka 35 hadi 40 ni karibu na 11.6% kwa jumla ya idadi ya waombaji.
Ambapo kiasi cha waombaji kutoka nchi za Kiafrika kilichangia sehemu kubwa zaidi ya idadi ya washiriki, kufikia karibu na 56.7%, wakati waombaji kutoka bara la Asia walikuwa karibu na 35.6%, wakati waombaji kutoka Marekani ya Kusini walikuwa karibu na 7.7% ya jumla ya waombaji.
Ikumbukwe kuwa fomu ya Uandikishaji ilifungwa Jumatatu 3/5/2021 saa Tano Adhuhuri, wakati ambapo Udhamini wa Nasser kwa uongozi ni mfano wa ushirikiano kati ya nchi za Kusini, kwani ni moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, pamoja na kile kilichozinduliwa kwa Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 12, 2019 (Siku ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano wa Kusini-Kusini) kufuatilia hivyo, katika toleo lake la pili, Udhamini huo ulichukua kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini" kukuza na kuboresha mawasiliano kati ya nchi zinazoendelea; linalosababisha ufahamu zaidi wa shida za pamoja na huongeza nafasi za kubadilishana maarifa na uzoefu upatikanao.

Comments