Misri yakaribisha Fainali za Kombe la Dunia la Tenisi kwa Wachipukizi


Shirikisho la Tenisi la Misri lilitangaza kuwa mwenzake, Shirikisho la Afrika, limeikabidhi Misri kuandaa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Tenisi ya vijana chini ya miaka 14 na 16.


Mechi hizo zinafanyika mnamo kipindi cha  21 hadi 27 Juni, kwa ushiriki wa timu 5 kwa kila awamu ya umri, kwa jumla ya timu 20 zikisimamishwa kwa Shirikisho la kiafrika na Shirikisho la Tenisi la kimataifa.


Misri imeshinda haki ya kuandaa kundi la tatu la Kiafrika kwa Kombe la Davis, litakalofanyika Agosti ijayo.


Bodi ya Wakurugenzi ya Shirikisho la Tenisi la Misri, linaloongozwa na Ismail El Shafei, limewateua Mhandisi.Walid Sami, Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Dokta Rasheqa Abu Shusha, na Mhandisi Mohamed Ibrahim, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, ili kuunda kamati ziandaazo, na kuanza maandalizi ya kuandaa mashindano kwa ufanisi wa hali ya juu na hatua kubwa zaidi ya tahadhari ili kutimiza mashindano kwa njia bora, kwa upande wa kiidara, kiufundi na kiafya.

Comments