Waziri wa Michezo ashuhudia hitimisho la Fainali za Sarakasi ya Afrika zinazofikisha Olimpiki ya Tokyo
- 2021-05-28 23:28:51
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, ameshuhudia, Alhamisi, hitimisho la mechi za Fainali za Sarakasi ya Afrika kwa Olimpiki ya Tokyo.
Misri inakaribisha mechi za Fainali za michezo ya Trampoline kwenye Ukumbi , namba 4 wa Uwanja wa Kimataifa wa Kairo, na Sarakasi ya kiufundi kwa wanaume na wanawake katika ukumbi wa Nasr City Club katika kipindi cha Mei 25 hadi 27.
Na leo, Wachezaji wawili wa timu ya kitaifa ya Misri, Malek Hamzah na Saif Aser, walifikia Olimpiki ya Tokyo, ili Misri ishinde kiti cha wasichana na wanaume katika Sarakasi ya Trampoline baada ya kushinda kwao kwa nafasi ya kwanza kwenye mechi za Fainali za Afrika zinazofikisha Olimpiki ya Tokyo 2020.
Nchi 7 zinashiriki katika mechi za Fainali za Kiafrika kushika Tiketi ya Tokyo 2020, nazo ni Algeria, Morocco, Cameroon, Afrika Kusini, Libya na Nigeria, pamoja na Misri, nchi mwenyeji.
Timu ya kitaifa ya Angola iliomba radhi kwa kutoshiriki mashindano hayo.
Ikumbukwe kwamba mashindano ya Afrika yanayofikisha Olimpiki ya Tokyo 2020, yanayokaribishwa sasa hivi kwa Misri , ni mazoezi ya mwisho kabla ya Misri kuandaa Kombe la Dunia la Sarakasi ya kiufundi Juni ijayo mapema, yanayofanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano barani Afrika.
Comments