Rais wa Shirikisho la Sarakasi azindua Michuano ya Kimataifa ya Kombe la Mafarao

 Ihab Amin, Mkuu wa Shirikisho la Sarakasi pamoja na Wakuu wa ujumbe ulioshiriki, walizindua mashindano ya kimataifa ya "Kombe la Mafarao" kwa mazoezi ya viungo kwenye Ukumbi wa Vijana na Michezo, huko mjini mwa Oktoba 6,  na yataendelea  kwa siku 3, kwa ushiriki wa nchi 12 nazo ni: Azabajani - Ukraine - Georgia - Moldova - Ugiriki - Hungary - Poland Italia - Lebanoni - Urusi - Uzbekistan - Misri ndiyo nchi mwenyeji "kwa jumla ya wachezaji 373.


 Mashindano hayo yanashuhudia hatua kali za tahadhari, kulinda wajumbe wanaoshiriki kutoka kwa virusi vipya vya Corona, Covid 19, na kusisitiza dharura ya kuzingatia maagizo ya kinga kutoka kwa Wizara ya Afya, wakati ambapo wajumbe wote walioshiriki katika mashindano wameshapata vipimo vya kimatibabu.


 Ihab Amin, Rais wa Shirikisho la Sarakasi,wakati wa hotuba yake, alithibitisha  kuwa Shirikisho lilitoa juhudi kubwa za kujumuisha mashindano kwenye Ratiba ya Shirikisho la Kimataifa la Sarakasi, akiashiria kuwa mashindano hayo yalichukua sifa rasmi baada ya kupata tathmini ya kimataifa kama ya Michuano ya kimataifa kwa Klabu.


 Amin ameshaongeza kuwa Misri ilifanikiwa kuangaza ulimwengu kwa kuandaa Kombe la Dunia la Sarakasi la kiufundi, lililofanyika kwenye mkusanyiko wa kumbi, huko Uwanja wa Kimataifa wa Kairo ndani ya 3 hadi 7 Juni hiyo, akitoa shukrani kwa Dokta. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Mhandisi Hisham Hatab, Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Misri

Comments