Waziri wa Vijana na Michezo awapokea ujumbe wa timu ya mpira wa mikono ya Misri kwenye Uwanja wa ndege wa Kairo
- 2021-08-13 22:11:57
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, amewapokea ujumbe wa timu ya mpira wa mikono ya Misri ikirudi baada ya ushiriki wake kwenye Michezo ya Olimpiki huko Tokyo.
Sobhy amesisitiza nia yake ya kuwapokea ujumbe wa mpira wa mikono wa Misri, haswa baada ya matokeo na nafasi iliyopatikana na wachezaji wa timu hiyo na wamepata nafasi yao ya nne.
Akiongeza kuwa nchi ya Kimisri, chini ya Urais wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kila wakati ni nia ya kuwalinda wanariadha wake na kuwatunza.
Ujumbe wa Misri ulishiriki kwenye Michezo ya Tokyo na wanariadha 137 kutoka michezo 25, wachezaji 89 wa kiume na 48 wa kike katika michezo: Mpira wa miguu, Mpira wa mikono, Upinde, Mishale, Silaha, Badminton, Tenisi ya meza, Taikondo, Kuogelea, Tenisi, Meli, Judo,Triathlon , Kupiga makasia, Kukanyaga, Kushindana, Mazoezi ya kisanii, Kuogelea kwa pamoja, Karate na Baiskeli, Pentathlon ya kisasa, Farasi, Kupiga mbizi, Ndondi na riadha.
Katika kikao hicho, ujumbe wa Misri ulishinda medali 6 mbalimbali, pamoja na medali za dhahabu, fedha na medali 4 za shaba.
Comments