Wizara ya vijana na michezo, kupitia utawala mkuu wa Majengo ya Vijana, ilitangaza kuwa Jiji la vijana huko Hurghada liko tayari kwa kufanya kazi na kuwapokea vikundi na shughuli anuwai katika Wizara baada ya kumaliza kazi zote za maendeleo ndani yake .
Hiyo inakuja kufuatia maagizo ya Dokta. Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na Michezo,kwa umuhimu wa kukamilisha miradi yote ya vijana na michezo, haswa miji ya vijana katika mikoa tofauti , kwa lengo la kuongeza viwango vya utalii wa ndani, kukamilisha utekelezaji wa Mpango wa " Jua Nchi Yako ”, na kukuza roho ya uaminifu ya vijana wa Misri .
Waziri huyo alisisitiza ufuatiliaji wa mara kwa mara wa miundombinu katika majengo ya vijana na michezo kote Jamhuri, ufuatiliaji wa shughuli zao mara kwa mara, na kufanya kazi kutoa mahitaji yanayotakiwa ya matengenezo au kuongeza ufanisi ili kuitunza kupitia idara husika ya Wizara, ambayo ni idara kuu wa majengo, kutilia mkazo kutoka kwa Wizara kwa kutoa huduma bora kwa Wachipukizi na vijana kikamilifu .
Sobhy aliashiria kuwa Misri ina muundo maarufu wa michezo ya vijana ulioenea katika mikoa yote, pamoja na vilabu, vituo vya vijana, miji ya michezo na vijana, kumbi za ndani, vituo vya elimu ya uraia na mabaraza ya vijana, akielezea kuwa majengo hayo yanalenga kuhudumia vijana katika kufanyika harakati za michezo, shughuli za vijana, utamaduni, sanaa na kijamii.
Jiji la vijana huko Hurghada lina uwezo wa watu 350, kwani lilijengwa katika eneo la ekari 20, na kuna ukumbi wa mikutano, kumbi za warsha, nyanja wa mpira, uwanja wa shughuli nyingi ukumbi wa mazoezi. Ndani ya Jiji hilo pia kuna pwani ya kibinafsi ambayo inaangalia moja kwa moja pwani ya Bahari Nyekundu.
Comments