Wizara ya Vijana na Michezo yaitoa Shukrani kwa Wizara ya Mambo ya nje kwa Ushirikiano wake kutatua mgogoro wa timu ya mpira wa kikapu ya wanawake
- 2021-08-17 13:20:23
Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, imepeleka barua za Shukrani kwa Wizara ya Mambo ya nje, ikiongozwa na Balozi Sameh Shoukry; Jitihada zilizofanywa kusuluhisha shida ya ujumbe wa wanawake wa mpira wa kikapu wa chini ya miaka 19, kushiriki katika Mashindano ya Dunia huko Hungary, mnamo kipindi cha kuanzia 4-16 Agosti hii.
Pia, Waziri wa Vijana na Michezo alimshukuru Balozi Amr El Hammamy, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri huko Ankara, Balozi Tarek Khalil, Balozi Mkuu wa Misri huko Istanbul, Rasha Al-Diyasti, Katibu wa Kwanza katika Ubalozi wa Misri huko Istanbul, na Mshauri / Engy Sharif Al-Samanudi, Chargé d'Affairs katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri huko Budapest, Hungary, Sekretarieti wa Pili / Khaled Essam Zaher, Balozi wa Misri huko Budapest, na pia wanachama wa Ubalozi wa Misri nchini Uturuki na Hungary; Hiyo ni kwa sababu ya bidii yao kubwa ya kupokea na makazi na kufanikisha mawasiliano mazito pamoja na Wizara ya Mambo ya nje ya Uturuki na Hungary na mamlaka katika viwanja vya ndege huko Istanbul na Hungary, na kwa kipekee, kupata Visa za ruhusa ya kuingia Uturuki na kisha Visa za kuingia Hungary.
Waziri huyo pia alihakikishia taratibu za kufikia timu hiyo nchini Hungary, pia maandalizi ya timu hiyo kushindana kwenye mashindano ya Dunia, yatakayoendelea hadi Agosti 16 huko Hungary, kwa kushirikiana na Dokta.Magdy Abu Freikha, Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri .
Mgogoro huo ulikuwa pamoja na Maandishi ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kimataifa yakisema kwamba ujumbe wa timu ya Misri hauna haja ya kupata Ruhusa ya kuingia ndani ya jimbo la Hungary wakati wa kufikia Uturuki, pamoja na Hungary, ukiongeza na Ujumbe huo wa kimisri umeshafika Uturuki, haukuweza kusafiri kwenda jimbo la Hungary kwa sababu haukuwa na Ruhusa ya kuingia kabla ya Kuondoka Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.
Comments