Waziri wa Michezo anaandaa chumba cha kati cha uendeshaji wa Kombe la Mataifa ya kiafrika kwa Soka.
- 2019-06-14 15:28:50
Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy, alikutana katika Chama cha Uendeshaji cha kati kilichoundwa kwa Wizara za Ulinzi,
Mambo ya Ndani, Mambo ya Nje, Umeme, Utalii, Usafiri, Vijana na Michezo,
Usalama wa Taifa, Ndege ya mashirika ya kiraia, Maendeleo ya kienyeji , Kituo
cha taarifa za Bodi la Mawaziri,
Afya,kameshina ya wagonjwa , Kampuni ya
Maji na Usafi.
Waziri wa Vijana na Michezo alisema kuwa chumba cha uendeshaji cha kati
kina lengo la kukabiliana na mgogoro wowote ambao unaweza kutokea kabla na
wakati wa michuano, akisisitiza kwamba jukumu lake ni muhimu kwa kushirikiana
na Kamati iandaayo.
Dokta Ashraf Sobhy alisema kuwa uanzishwaji na uundaji wa Kituo cha
Uendeshaji wa kati unasisitizia mfumo
mkuu wa kiidara ambao michuano inategemea
kulingana na mtazamo wa uongozi wa kisiasa , na mielekeo ya Rais wa Jamhuri ili kushinda vikwazo
vyovyote vinavyoweza kuzuia kazi yoyote
inayohusiana na michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Soka.
Sobhy aliendelea kuwa kazi hiyo inaendelea kati ya vyama vyote
vinavyohusika, ili kufanikiwa michuano ,na kuitoa kwa njia inayofaa jina na
sifa ya Misri.
Comments