Mawaziri wa Michezo wa Misri, Algeria, Nigeria na Ghana wajadili mifumo ya Ushirikiano wa vijana na michezo Barani Afrika
- 2021-10-03 20:07:18
Pembezoni mwa shughuli za mkutano mkuu wa Shirikisho la Kamati la Olimpiki za Kiafrika "EL ANOKA" inayofanyika nchini Nigeria, mkutano wa kiwizara wa pande nne uliofanyika katika Uwanja wa Kitaifa wa Mocho Abiola katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kati ya Dk Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo , Sunday Dayr Waziri wa Vijana na maendelezo ya Michezo ya Nigeria , Abdelrazik Sabak Waziri wa Algeria wa vijana na michezo na Mustafa Youssef Waziri wa Vijana na Michezo wa Ghana.
Mkutano huo ulifanyika kutokana na juhudi za pamoja za kuboresha uhusiano na kuimarisha ushirikiano katika nyanja za vijana na michezo kati ya Misri , Nigeria, Ghana na Algeria, kupanga mipango na shughuli kati yao na kujenga upeo mpya wa ushirikiano.
Mkutano ulijadili nyanja zenye masilahi ya pamoja na njia za ushirikiano zinazoonekana katika kufundisha na kutoa maarifa ya ustadi wa dijiti, mashindano ya pamoja na maendelezo ya michezo, mafunzo na kuunga mkono kuendeleza miradi na ujasiriamali, na mipango ya kubadilishana vijana kati ya nchi nne.
Imeshakubaliwa kuunda kamati ya kiufundi ya wataalam ili kuandaa programu ya utendaji kwa nyanja za ushirikiano, zinazojumuisha wanachama wa watu 16, na wawakilishi 4 kutoka kila nchi, na kuidhinisha kamati hiyo kwa ajili ya kuandaa mipango ya ushirikiano na njia za utekelezaji kulingana na ratiba maalum , baada ya kufanyika mkutano wa ukaguzi wa kiufundi wa mwisho nchini Algeria mnamo Novemba ijayo, ikiwa ni maandalizi ya kukubaliwa na nchi hizo nne, ili kuimarisha ushirikiano wa vijana na michezo Barani Afrika.
Comments